SITAKI kudai kuwa najua kwa uhakika sababu za Kamati
ya Usalama na Maadili kukata jina la Edward Ngoyai Lowassa kutoka katika
orodha ya wagombea wa urais ambao majina yao yaliwasilishwa katika
Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa kwa ajili ya mchujo.
Lakini si vigumu sana kudodosa kwa nini kampeni ya Lowassa iliangukia pua. Lowassa alifanya makosa kadhaa ya kimkakati.
Ili kuelewa kilichomfanya Lowassa kufanya makosa hayo ya kimkakati, ni
muhimu kupitia muktadha wa historia ya Lowassa kisiasa. Kuna mambo
mawili ya msingi katika muktadha huu.
Kwanza, Mwalimu Nyerere alihoji usafi wa Lowassa na inadaiwa alimkataa
wakati wa uhai wake asigombee urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutokana na utajiri mkubwa usioelezeka.
Pili, Lowassa alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008 baada kashfa
ya Richmond iliyohusiana na mkakati wa Serikali wa kutafuta njia za
dharura za kutatua tatizo kubwa la uhaba wa umeme.
Hicho ndio cheo chake cha mwisho kikubwa cha kisiasa. Ndoto za Lowassa, ambaye aliamini angedumu katika wadhifa huo kwa miaka 10 yote ya Kikwete na hatimaye kumrithi nafasi ya urais, zilizimika ghafla.
Watu wawili wanatajwa kuwa ni nyota wa sinema ile ya kisiasa, ya Richmond, iliyomdondosha Lowassa. Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe na Spika wa Bunge wa wakati ule, Samuel Sitta. Si ajabu basi kuwa wawili hawa wamebakia kuwa ni maadui wa kisiasa wa Lowassa.

Baada ya kustaaafu, kumekuwa na tetesi kuwa uhusiano wa Lowassa na
rafiki yake wa karibu wa siku nyingi, Jakaya Kikwete umekuwa ukiyumba
huenda labda kwa sababu Lowassa anaamini hakutetewa. Wapo hata
wanaoamini kuwa Kikwete alikuwa nyuma ya mkakati wa kumuondoa kutokana
na ‘spidi’ kali ya utendaji ya Lowassa iliyotishia kumfunika.
Katika muktadha huo, urais kwa Lowassa ungekuwa na maana mbili kubwa.
Kwanza, ingekuwa ni nafasi ya kusafisha jina lake kwa sababu kwa kawaida
ni matendo yetu ya mwisho ndiyo yanayojenga urithi wa namna
tutakavyokumbukwa. Nafasi ya juu ya Lowassa serikalini ilikuwa ni
uwaziri mkuu ambao aliuacha kwa kashfa akituhumiwa kufisidi.
Pili, kwa Lowassa hii ingekuwa nafasi ya kulipa kisasi kwa wabaya wake.
Wapambe walidai hana visasi, lakini je angemteua Mwakyembe, Sitta au
Paul Makonda kushika nafasi yoyote Serikalini.
Nina hakika, utawala wa Lowassa ungehitimisha au kufifisha mustakbali wa kisiasa wa wanasiasa hawa katika uongozi wa nchi hii.
Nina hakika, utawala wa Lowassa ungehitimisha au kufifisha mustakbali wa kisiasa wa wanasiasa hawa katika uongozi wa nchi hii.
Hakuna haja ya kukaza mishipi ya shingo kupinga ukweli huo kwa sababu
Lowassa asingekuwa wa kwanza kufanya hivyo. Ukichunguza utagundua kuwa
hata Nyerere, Mwinyi, Kikwete – wote waliwanyima fursa baadhi ya watu.
Watawala wote wanafanya hivyo na si vibaya kufanya hivyo, kisiasa.
Akijua kuwa angekamilisha mawili hayo, kusafisha jina na kulipa kisasi,
Lowassa aliutaka sana urais. Kuutaka sana si tatizo. lakini kuonyesha
kuwa anautaka sana ilikuwa ni tatizo. Ilikuwa ni suala la ‘iwe isiwe’,
‘vyovyote iwavyo’ na ‘kwa gharama yoyote’. Ilitutisha baadhi ya watu. Na
hilo lilikuwa kosa la kwanza alilolifanya.
Katika kuutaka sana urais, Lowassa kiaina alitoa ‘ultimatum’ (tishio) kwa chama chake. alinukuriwa akisema haoni uwezekano wa kushindwa na haoni mtu wa kumkata jina lake.
Katika kuutaka sana urais, Lowassa kiaina alitoa ‘ultimatum’ (tishio) kwa chama chake. alinukuriwa akisema haoni uwezekano wa kushindwa na haoni mtu wa kumkata jina lake.
Hilo lilikuwa ni kosa jingine. Alikiuka msingi muhimu wa CCM ambao
wenyewe wamekuwa wakiukariri mara kwa mara, ‘chama kwanza, mtu baadaye’.
Ni wazi kuwa kama angekuwa Rais, ingekuwa ngumu kwa CCM kumdhibiti. Angekuwa na nguvu kuliko chama. Haipaswi kuwa hivyo, hususan, sasa wakati ambao Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana anamikakati ya kukipa chama nguvu zaidi za kusimamia Serikali.

Lowassa akaendelea kufanya kosa jingine la kukaribisha marafiki na
wapambe wenye tuhuma na tabia za kutia shaka katika kampeni yake.
Miongoni mwa hao walikuwapo mawaziri wa zamani na wafanyabiashara
waliotoka serikalini kwa kashfa mbalimbali.
Haikuwa hatua nzuri kwa Lowassa ambaye tayari ana doa la Richmond kujizungushia atu wenye madoa kama yeye.
Hata watu waliojitokeza hadharani kuhoji uamuzi wa Kamati Kuu,
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake Sophia Simba, Mwenyekiti wa zamani wa
Jumuiya ya Vijana wa CCM, Emmanuel Nchimbi na mbunge wa Afrika ya
Mashariki, Adam Kimbisa, kwa maoni yangu waliongozwa na maslahi yao
kuliko ya watu. Hakuna kati yao mwenye rekodi safi ya kuonyesha
anasimamia maslahi ya umma. Kwangu hawa wote ni ‘opportunists’.
Kampeni ya Lowassa pia ilikuwa ya kitajiri. Pesa zilikuwa nje nje hadi ikawa ni ngumu kujua nani anamfuata Lowassa kwa sababu ya pesa na nani anaamini kwa dhati katika ubora wa urais wa Lowassa kwa ajili ya maendeleo!

Baadhi ya waandishi wa habari walineemeka mno katika kipindi hiki na
ulikuwa muda mzuri kwa wenyeviti wa mikoa wa CCM kuchuma hadi wakajitoa
‘akili’ na kuonyesha wazi mapenzi yao. Hata Mwenyekiti wa Geita,
anakotoka Magufuli, alikuwa kambi ya Lowassa!
Katika kuonyesha nguvu ya pesa tulishuhudia masheikh na wachungaji wenye
njaa na mabodaboda waliokata tamaa wakienda kumshawishi agombee –
usanii mtupu! Maandalio ya nguo na vifaa vingine vya Timu Lowassa
yalikuwa makubwa mno – hata kabla hajajua kama atapita katika mchujo!
CCM kumteua Lowassa ingeweza hata kukiletea chama hicho hatari kwa
sababu wapo wanaodhani mgombea huyo alikiuka si tu kanuni za maadili za
chama, bali pia sheria za uchaguzi. Ikumbukwe msajili wa vyama vya siasa
nchini, Jaji Francis Mutungi alishaonya kuhusu kuzingatia sheria ya
gharama za uchaguzi inayothibiti matumizi mabaya ya fedha katika
mchakato huo.
Lowassa, akijua hatari anayokabiliana nayo kutoka kwa wahafidhina ndani
ya chama waliohoji maadili yake, akaamua kuja na mkakati wa kuunda
‘kundi la msukumo kutoka nje ya chama’ ili wahafidhina wafanye uamuzi
kwa shinikizo. Haukuwa pia mkakati mzuri sana na kinyume na matarajio
uliimarisha azma ya wahafidhina ya ‘kumkata’.
Hata hivyo, makosa ya kimkakati aliyoyafanya Lowassa yanaeleweka.
Alikuwa na kazi mbili ya kuzuia na kushambulia na akatumia mkakati wa
kutumia maguvu mengi kuliko akili. Hatimaye ikamgharimu.
Lakini Lowassa angefanyaje? Jibu rahisi ni kuwa angekuwa mnyenyekevu kitabia, angetengeneza timu ya watu wasafi, angefanya mambo kwa kiasi na chinichini. Wazungu wanasema, ‘ chochote kikizidi sana kinadhuru’.

Kilichomponza Membe…
Binafsi sikutarajia kwamba Membe angepita katika mchujo, wakati Lowassa amekatwa. Nilitarajia kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ingeona busara ya kukata jina lake (Membe) ili kuvunja makundi na kuleta umoja katika chama.
Nani asiyejua kuwa Membe ndiye aliyekuwa mpinzani wa moja kwa moja wa Lowassa? Hawa ni kama Simba na Yanga.

Kotowiva kwa kwa kambi ya Lowassa na Membe hakukuja hivi hivi. Timu ya
Lowassa iliamini kuwa Membe ni mtu wa karibu wa Kikwete na ndiye chaguo
la Ikulu. Kwa hiyo timu ya Lowassa iliamini juhudi za Ikulu kumkata
mgombea wao zililenga kumsaidia Membe.
Kutokana na ukaribu unaozungumzwa wa Kikwete na Membe, ambao ni kama
mashemeji ukizingatia Membe anatoka Lindi kama mama Salma, haikuwa ngumu
kwangu kutabiri kuwa Membe angeanguka katika Halmashauri Kuu ya Taifa
ambayo ilijaa wapenzi wa Lowassa.
Kadhalika, haikuwa ngumu kung’amua kuwa kijana mwingine wa Kikwete,
mwandishi wake hotuba wa zamani, Januari Makamba angeungana na Membe
kutupwa nje ya kinyang’anyiro. Ukaribu wao na Kikwete uliwaponza wawili
hawa.
Katika ‘saga’ la Lowassa, sitaacha kuhoji kuhusu misimamo ya Kingunge
Ngombale Mwiru, mwanasiasa mkongwe, ambaye kabla ya matukio haya
nilimweka katika kiwango cha uadilifu, umahiri na heshima cha Nyerere,
Kawawa na waasisi wengine.
Kwa nini alikubali kujipaka matope na kuondoa heshima yake kwa sababu ya Lowassa? Aliahidiwa nini hadi akajitokeza hadharani kama muasi na kujaribu kuaminisha watu kuwa CCM itashinda tu kama Lowassa atakuwa mgombea? Yule si Kingunge niliyemfikiria alivyo.

Magufuli aokota dodo…
Mwisho wa siku mwanakemia John Magufuli, aliyeendesha kampeni ‘poa’ ya bila mbwembwe, akaokota embe dodo mchangani katika Mkutano Mkuu wa CCM baada ya kuwadondosha wanawake wawili Amina Salim Ally na Asha Rose Migiro ambao aliingia nao fainali katika kinyang’anyoro hicho.
Sina hakika kama anastahili zaidi kuliko wagombea wote lakini bila shaka alikuwa chaguo bora kuliko akina mama wawili alioingea nao fainali, ukizingatia changamoto zinazolikabili taifa na changamoto ya vyama vya upinzani.

Magufuli anatoka Kanda ya Ziwa. Yeye ni mtendaji mzuri anayetaka kuona
matokeo, ana uzoefu usiopungua miaka 20 serikalini. Pamoja na kuwa ni
mwanasayansi, Magufuli ni mwanasiasa mahiri jambo lililothibitika kwa
jinsi alivyokuwa akichangamana na watu katika Mkutano Mkuu ukumbini hapo
akiomba kura.
Magufuli ana udhaifu wake pia. Hajui Kiswahili na anachanganya ‘r’ na ‘l’ katika matamshi yake. Wakati fulani anaweza kuwa dikteta. Pia Magufuli ana maamuzi ya haraka. Naamini hana uzoefu mkubwa kimataifa na labda atawahitaji wazoefu kama Amina Salim Ally, Asha Migiro na Dk. Augustine Mahiga, kumsaidia katika eneo hilo.

Hata hivyo, ukweli ni kuwa changamoto nyingi zinazokabili Taifa kwa sasa
ni za ndani zaidi kuliko nje. Tunatarajia Magufuli akipitishwa kuwa
rais ataimarisha mshikamano wa Taifa, atapambana na rushwa na ufisadi,
ataanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya, ataleta nidhamu katika
ukusanyaji wa mapato ya Serikali na matumizi.
No comments:
Post a Comment