18 July, 2015

Nay wa Mitego: Nina Maana Yangu Kutumia Damu Kwenye Video Zangu

Akizungumza na Clouds E ya Clouds TV, Nay amesema bado kuna video zinakuja zitakazokuwa na damu.
“Hii ni video ya pili naifanya hivi na kutakuwa na video nyingine ya tatu ambayo itakuwa na vitu kama hivyo,” alisema. “Hii ni kama sign yangu, kwahiyo nimepokea maoni mengi kuhusu kufanana kwa hii video lakini yote ni kwaajili ya damu na damu ni kama nilivyosema hii ni sign yangu,” aliongeza.

Pia Nay alieleza sababu iliyofanya wimbo wake na Diamond, Mapenzi au Pesa kufeli.

“Ndio haujafanya vizuri lakini tukumbuke wimbo Mapenzi au Pesa ni wimbo ambao umekosa video. Kwenye muziki wetu wa siku hizi watu wanataka video haraka, ukichelewa kufanya video wimbo unakuwa unapungua kasi siku hadi siku. Tumeshaona hili kwenye nyimbo nyingi sana za wasanii wetu, ukichelewa kutoa video, wimbo unakufa haraka sana, yaani unakuwa unapungua nguvu siku hadi siku.”

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...