Waziri wa Miundombinu nchini
Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame siku ya Jumamosi, Julai 18 2015
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Magufuli baada ya kufungua rasmi
michuano hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya
Kagame, mechi itakayowakutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya
Yanga dhidi ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.
Michuano ya Kagame inatarajiwa
kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, ukindoa mecho
ya Yanga Vs Gor Mahia, mechi zingine zitakua ni kati ya APR dhidi ya Al
Shandy uwanja wa Taifa saa 8 mchana, KMKM Vs Telecom saa 10 jioni uwanja
wa Karume.
Kuanzia leo tutakua tunawaleta kwa ufupi timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu, na kwa kuanza tunaanza na kundi A;
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment