Akizungumza na Bongo5 leo, Linah amesema mwanaume aliye naye kwa sasa ni
mwanaume aliyekuja kumuokoa akiwa katika wakati mgumu wa kimapenzi.
“Kiukweli malengo yetu ni ndoa na wala haitachukua muda mrefu. Mungu
akijalia mwakani,” amesema Linah. “Sasa hivi nataka ndoa mambo ya kuzini
sitaki. Mimi sidhani kama ndoa ina ugumu wowote. Nataka sasa hivi kuwa
wa halali kwa mtu mmoja na baadaye tupate watoto. Kwa jinsi tulivyoongea
kazi ni kazi na mapenzi ni mapenzi, kwahiyo nafasi yangu ya kazi
itakuwa pale pale. Na ninafikiri huyu ni mtu sahihi kwangu, ninafikiri
ni mtu ambaye anaweza akawa mume wangu ndio maana nimekimbilia ndoa,”
ameongeza.
“Amekuja kwangu kama mtu anayenipenda, ameona jinsi ninavyoumia
kimapenzi. Kwahiyo huyu amekuja kama mtu mwenye nia, ni aina ya mwanaume
ambaye nilikuwa namtafuta kwa muda mrefu na hatimaye amefika, sasa hivi
nafurahi.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment