Man United wameweka masharti
kwamba De Gea atauzwa Real Madrid majira haya ya kiangazi endapo miamba
hiyo ya Bernabeu itakubali kuwauzia mlinzi wa kati, Sergio Ramos.
Kumbuka De Gea na Ramos wote wapo katika timu zao kujiandaa na msimu mpya.
Kocha mpya wa Real Madrid, Rafa
Benitez amesema hataki tu Ramos abakie Bernabeu bali anataka kumpa
kitambaa cha unahodha kufuatia Iker Casillas kuondoka.
Kwa mujibu wa The Guardian,
inasemekana dili la Ramos kutua Old Trafford linaweza kukamilika kabla
ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Majira ya kiangazi.
United hawana presha ya kuuza
wachezaji kwenda klabu kama Real Madrid kwasababu wana mkwanja wa
kutosha kuweza kuwazuia wanasoka wake.
No comments:
Post a Comment