16 July, 2015

BASTIAN SCHWEINSTEIGER AMEKULA DILI LA BEATS by DRE BAADA YA KUHAMIA MANCHESTER UNITED

cccc
Hapa shabiki wa Manchester united anaweza kuimba line ya John Makini “Brand kubwa sio kitoto”. Baada ya Bastian Schweinsteiger kuhama kutoka Bayern Munich amehamia Manchester united wahusika wa masoko wa brand ya Beats by Dre wametumia fursa ya uhamisho wake kwenye biashara yao.
Hivi sasa limetoka tangazo ambalo linamuonyesha Bastian Schweinsteigerakihama kutoka Berlin kueleka Manchester ambapo Bastian Schweinsteiger anaonekana anafungasha mizigo yake. Kwenye hiyo process Bastian Schweinsteiger anavaa headphones za Beats by Dre. So hawa jamaa wameona kwamba Manchester ni brand kubwa ina mashabiki wengi, kumhusisha mchezaji mwenye jina kubwa Bastian Schweinsteiger akihamia Manchester united ni rahisi kwa brand yao kupata wateja wapya ambao ni mshabiki wa Man United.
Sio uongo wala sio hasara, pesa walizomplipa Bastian Schweinsteiger zinaweza kurudi kwasababu tangazo lake limeshaangaliwa mara milioni 3 mbalimbali duniani. Mitandao karibia yote duniani ya michezo pamoja na shaffhdauda.co.tz wameandika habari hii. Bila shaka Beats by Dre wanapata matangazo ya bure kupitia Bastian Schweinsteiger.
Pia kuna mashabiki wa Manchester united hivi sasa wanafikiria kwenda kununua headphone hizi sio kwamba wamesikia ni nzuri bali ni kwasababu Bastian Schweinsteiger amehusika ku-promote. Mpira wa bongo lini huku. Mchezajji mkubwa akihamia most valuable club biashara sio kuuza jezi tu, mambo ndio kama haya.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...