Zaidi ya kuwa na kipaji kimoja mtu anaweza kuwa na kipaji kingine au passion na kitu kingine tofauti na kile kinachompatia pesa kila siku.
Swala hili limedhihilika kwa mchezaji wa Manchester city Gael Clichy. Huyu jamaa hata akisafiri lazima abebe Dj Set up ili akifika huko anapoenda kama sehemu moja wapo ya starehe yake anaanza kufanya mixing ya ngoma mbalimbali.
Akiojiwa na Manchester TV wakati wapo kwenye moja ya majiji waliyotembelea kwenye pre-season tour, Gael Clichy alisema huwa habebi vitu vingi akiwa kwenye safari lakini hawezi kuacha DJ set up zake.
No comments:
Post a Comment