16 July, 2015

IJUE VIZURI SIMU YA HUAWEI P8 KABLA HAUJAINUNUA

PPP
Jana kwenye hoteli ya Hyatt Regency kampuni ya Huawei inayouza na kuzalisha “simu zenye akili”a.k.a SmartPhone ilizindua toleo jipya la simu zake kwenye P Series. Baada ya watu mbalimbali kufurahia P7, hivi sasa ni wakati wa kutumia P8. Hizi hapa ni sababu za kutosha kabisa zitakazo kufanya uimiliki  simu hii ya Huawei P8.
Battery:
Ukizungumzia matatizo ya Smartphone hili ni moja wapo, huwezi kuniambia niache kusikiliza music na kuchat kwa pamoja kisa battery. Kila mtu anaitaji kufanya vitu mbalimbali kwa wakati mmoja kwenye smartphone yake. Director of Sales and Marketing Samson Majwala amesema kwamba battery ya Huawei P8 inauwezo wa kukuwezesha kufanya yote na kukaa kwa siku nzima na chaji. Battery lake halitoki kwenye simu na lina uwezi mkubwa wa Li-Po 2680 mAh
p5
Camera:
Smartphone bila camera kali bado haijawa smart, Huawei P8 inakuja na camera yenye mega pixel 13 (4160 x 3120 pixels) zaidi ya hapo camera hiyo ina uwezo wa Autofocus, optical image stabilization, dual-LED (dual tone) flash. Haijaishia hapo, bali ukiwa unapiga picha uweza kufanya Geo-tagging, touch focus, face/smile detection, panorama na HDR.
Vipi camera ya selfie, hapo unakutana na camera yenye uwezo wa 8 mega pixel na 1080p. So Huawei P8 inakupa uwezo wa kurekodi video ya High Definition ya 1080p@30fps.
p17
Umbo:
Samson Majwala anaendelea kusema kwamba mara nyingi tuvaa nguo ambayo imetu-fit vizuri na hatutaki mizigo mingi kwenye mifuko yetu. Ukiizungumzia Huawei P8 ni nyembamba na bado ni ngumu hata ukiiweka mfukoni sio rahisi kukusumbua. Ina vipimo vya 144.9 x 72.1 x 6.4 mm. Uzito wake ni 144 g (5.08 oz) na nyembamba kwa 6.4mm
Sim Card
Huawei inakupa machaguo mawili kwenye swala la simcard. Zipo Huawei P8 zenye line moja na nyingine zina line mbili.
Operating System
Kama kawaida Huawei huwa inatumia O.S ya Android, lakini Huawei P8 sio tu kutumia Android bali inatumia Android mpya kabisa ambayo ni version 5.0.2 (Lollipop).
p2
Speed
Hakuna anetaka kufungua camera na kuisubili sana kufunguka au kufanya kitu chochote kwenye simu yako na ikawa slow. Huawei P8 imezingatia hilo kwa kuipa uwezo wa Quad-core 2 GHz Cortex-A53 & quad-core 1.5 GHz Cortex-A53. Pia Ram ya Huawei P8 ni 3GB ambayo ni RAM inayozidi hata baadhi ya laptop.
Memory
Mfano kama picha inapigwa na camera ya 13 mega pixel basi lazima inahitajika memory ya kutosha kuhifadhia picha,video na mafaili mengine. Huawei P8 inaweza kuwa na memory ya 16GB au 64GB na pia kwa speed yake unaweza kuongeza memory card hadi yenye 128GB na simu ikabaki kwenye ubora wake.
20150715152416
Mr Samson Majwala (Huawei Director of Sales & Marketing) na Peter Zhang Huawei Country Manager
Network
Huawei P8 imepewa uwezo mkubwa wa kudaka network ya mtandao wako wa simu. Mr Majwala anasema kuna wakati simu inavyobadilisha mnara, inawezekana kuwepo na delay kidogo. Lakini simu hii inauwezo wa kudaka haraka network na sio rahisi kupiga simu na isiunganishwe na mtandao. Pia inawezo wa haraka wa kudaka WiFi. Smartphone hii a.k.a simu yenye akili inauwezo wa kuchagua WiFi ambayo ina nguvu sana kwa wakati huo.
Ziada
Vitu vya ziada ni kwamba ukiwa unataka ku-screenshot kwenye Huawei P8 basi kazi ni rahisi sana. Una doubletap screen na utakua umesha screenshot.
p1
Director’s mode : Kwenye Huawei P8 unaweza kurekodi video kwenye angle 3 na ukawa una mix hizo video wakati unarekodi kama dirrector na mwisho siku ukapata video iliyokua mixed vizuri kama na director.
Huawei P8 ni ngumu imetengenzwa kwa design nzuri ya kuvuti ikiwa na cover la chuma ngumu kulinda simu yako vizuri.
Unaipataje?
Huawei P8 lazima itakua kwenye maduka muhimu ya kuuzia simu. Ukitaka yenye line mbili ni Tsh 1,200,000 na ukitaka yenye line moja ni Tsh 1,100,000

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...