Bada ya mlinda mlango wa zamani
wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Juma Kaseja kusaini mkataba wa miezi sita
kujiunga na timu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya, kipa huyo mkongwe
ameweka wazi ni kwanini amejiunga na timu hiyo ya wagonga nyungo wa jiji
la Mbeya wakati kulikuwa na vilabu vingi vikiiwinda saini yake.
Kaseja amesema, kikubwa
alichoangalia kabla ya kuamua kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya
Mbeya City ni ushindani wa klabu atakayokwenda kucheza kwenye ligi kuu
Tanzania bara na baadae kuamua kujiunga na Mbeya City.
“Kwanza nachoweza kusema ni
kwamba, naviheshimu vilabu vyote, naiheshimu Coast, African Sports,
Ndanda, Mwadui na timu zote zinazocheza ligi kuu ni timu kubwa kwahiyo
zote naziheshimu. Nilijaribu kuwa mtulivu kwa kipindi chote hiki
kuangalia ni timu ipi nitaenda kucheza ambayo itakuwa na ushindani
mkubwa”, amesema Kaseja.
Kaseja anaesubiri kujumuishwa
kwenye kikosi cha Mbeya City amewaomba wachezaji wenzake wa kikosi hicho
pamoja na mashabiki wa timu hiyo kuwa na muungano, umoja na amani ili
kuifikisha timu yao pale ambapo kila mwana Mbeya City anataka timu hiyo
ifike.
Hapa chini nimekuwekea stori nzima ya Kaseja wakati akifanya mahojiano na Shaffih Dauda, bofya hapo kusikila kila kitu….
No comments:
Post a Comment