19 August, 2015

KOCHA MSAIDIZI AZAM AKUBALI YAISHE…

NsimbeAliyekuwa kocha msaidizi wa Azam FC George Nsimbe Best ametimka kunako klabu hiyo baada ya makubaliano ya pande hizo mbili kuafikia muafaka wa kufanya hivyo ambapon tayari kocha huyo wa zamani wa klabu ya KCCA FC ya Uganda amesharejea nyumbani kwao Uganda.
Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd Maganga amehibitisha kuondoka kwa Nsimbe ndani ya Azam na kusema nafasi yake imechukuliwa na Romano ambaye atakuwa akimsaidia kocha mkuu wa timu hiyo Stewart Hall.
“Ni kweli mwalimu George Best hatuko naye, alikuwa ni mwalimu msaidizi kwenye timu yetu lakini mchezo wa mpira una kuingia na kutoka, amekaa na uongozi wamezungmza na wamekubaliana hatimaye George Best merejea Uganda na Romano ndiye amechua nafasi ya ukocha msaidizi kumsaidia Stewart Hall kwa kipindi hiki”amesema Maganga.
Nsimbe alipewa majukumu ya kuinoa Azam kwa muda mara baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa kipindi hicho, Joseph Omog kutimuliwa kwenye nafasi hiyo mwezi Februari mwaka huu kufuatia kuondoshwa kwa timu hiyo kwenye michuanon ya vilabu bingwa barani Afrika na timu ya Al Merreikh ya Sudan.
Kocha huyo alikisaidia kikosi cha Azam kumaliza kikiwa nafasi ya pili nafasi ambayo ilikuwa ikigombewa pia na ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba.
Baada ya Azam kuamua kumrejesha kocha wao wa zama Stewart Hall, Nsimbe alirudishwa chini na kuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho chini ya Muingereza Hall ambaye ndiye aliyekabidhiwa mikoba ya ukocha mkuu wa matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...