Memphis Depay amechukua headline ya mechi ya jana lakini pia kwenye takwimu mkongwe Bastian amefanya kazi kubwa licha ya kuingia kipindi cha pili.
Katika dakika 45 alizocheza Bastian amepiga pasi nyingi zaidi ya mchezaji yoyote wa Club Bruges ambae amecheza dakika zote 90.
Pia amewatia aibu wachezaji wenzake ambao walikua wanacheza tangu mwanzo wa mechi kwa kupiga pasi nyingi zaidi yao. Mfano Wayne Rooney,Memphis Depay na Adnan Januzaj. Bastian amepiga jumla ya 54 ndani ya dakika 45 alizocheza.
Wastani ni kwamba kila dakika ya mchezo alikua anapiga pasi kwenda kwa mchezaji mwenzake ili waende kutupia nyavuni. Hii inaonyesha jinsi gani alikua busy uwanjani na kuchangia ushindi wa 3 – 1.
No comments:
Post a Comment