20 August, 2015

Ben Pol akiri alipitia kwenye wakati mgumu baada ya kutoka MLAB

Muimbaji wa Sophia, Benard Paul aka Ben Pol amedai kuwa baada ya kuisha mkataba na kampuni ya MLAB iliyomweka kwenye ramani, alipitia wakati mgumu hadi kuweza kusimama mwenyewe.

Akiongea hivi karibuni kwenye kipindi cha Chill na Sky, Ben Pol alisema changamoto kubwa iliyomkabili baada ya kuchana na MLAB ni njia za kusambaza kazi zake.

Anasema wimbo wake Number One Fan ulipotoka alijikuta akiwapa watu wachache tu kwakuwa hakuwa akijuana na watu wengi tofauti na mwanzo ambapo MLAB ilikuwa ikifanya kazi hiyo yenyewe.

“Lakini ule wimbo ulienda wenyewe hadi mpaka next year ukapata nomination ya Best RnB song,” alisema msanii huyo.

Wimbo huo ulishinda tuzo hizo za KTMA mwaka 2012 bila kutarajia.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...