20 August, 2015

Joketi Mwegelo ‘Kidoti’ awataka wasanii wakike wanunue bidhaa zake badala ya maneno matupu tu!

MWANAMITINDO, Joketi Mwegelo ‘Kidoti’, amewataka wasanii wenzake hasa wa kike wamtie nguvu kwa kununua bidhaa zake badala ya maneno matupu.

Mrembo huyo ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, alifafanua kwamba wasanii wengi wa kike wamekuwa wakisifia bidhaa zake kwa maneno lakini hawamuungi mkono kwa kuzinunua.

Jokate ambaye pia ni mwanamuziki na mwigizaji, alisema wasanii hao wakitumia bidhaa zake zitamuongezea kipato na kumtangaza yeye pamoja na taifa kwa ujumla kwa kuwa wasanii hao wana majina makubwa ndani na nje ya nchi.

“Wapo wasanii wanaonunua kazi zangu kwa wingi lakini wengine wanaahidi tu hawanunui, nawaomba wanunue ili tusaidiane kuzitangaza na pia tutangaze taifa letu kwa ujumla kutokana na nafasi na majina yetu yalivyo makubwa ndani na nje ya nchi,’’ alisema.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...