19 August, 2015
CHELSEA YAIPIGA TOBO MANCHESTER…PEDRO KUSAINI NA CHELSEA MUDA WOWOTE
Katika kile kilichotafsiriwa kama ni Van Gaal kupigwa tobo na Jose Mourihno katika harakati za kumsajili Pedro, imekua ni habari ya kushtukiza sana kwa mashabiki wa Manchester tofauti na walivyotegemea. Hadi mara ya mwisho kila mtu alikua anajua kwamba Pedro atacheza kwenye kikosi cha Manchester United, lakini mambo yanaenda kombo.
Licha ya kumtuka vice chairman wao Ed Woodward mtu maarufu kabisa kwa kufanya madili yanayoipa faida Manchester, lakini muda huu anaonekana kuwa amechemsha. Habari ni kwamba pesa kiasi cha pound milion 21.1 zimetumika kusamjili Pedro kujiunga na Chelsea ikichangiwa na ushawishi mkubwa wa mmiliki wa Chelsea Abramovich.
Pedro alionekana kutokulidhishwa na Manchester baada ya Chelsea kumpa dili la £19m wakati United walitoa £17m.Siku ya leo ndio inategemewa Pedro atadondoka wino na kuwa Team Blue rasmi. Chelsea wanaonekana kutumia kwa nguvu sana muda huu uliobaki kusajili wachezaji kutokana na kuanza vibaya na kusitasita kwenye harakati za kutetea ubingwa wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment