Wayne
Rooney amesema yuko tayari kuwa mfungaji bora wa Manchester Unites kwa
mara nyingine na amewapa changamoto wenzake ya kuandika Historia msimu
ujao.
Nyota
huyo wa England alicheza namba nyingi msimu uliopita chini ya Louis van
Gaal na ikifika wakati akashushwa mpaka kiungo cha chini.
Kwasasa Rooney anataka kucheza namba anayoipenda yaani namba 9 na amesema yuko tayari kufunga magoli.
“Niko
tayari kubadili akili yangu na kuwa moja ya wafungaji wa magoli,”
Amesema nyota huyo wa zamani wa Everton ambaye msimu uliopita aliifungia
United magoli 12.
“Nataka kucheza nafasi ya mshambuliaji ambapo nadhani ninaweza kufunga, naamini naweza kulitekeleza hilo”
Msimu
wa 2009-10 na 2011-12, Rooney alifunga magoli 34 kwenye mashindano yote
akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati na kama atarudishwa nafasi hiyo
anaweza kufanya vizuri.
Siku
za karibuni, kocha wa Man United, Louis van Gaal alisema anatarajia
kumtumia Rooney kama mshambuliaji wa kati msimu ujao na maneno haya ya
Wayne ni majibu kwa bosi wake.
No comments:
Post a Comment