Klabu ya Manchester City imeshuka dimbani leo hii kucheza mechi yake ya kwanza ya michuano ya International Champions Cup dhidi ya AS Roma ya Italia… Michuano hiyo inayoandaliwa na Audi inafanyika Australia katika Uwanja wa Melbourne Cricket Ground na kushirikisha jumla ya timu tatu za Real Madrid, AS Roma na Man City.
Man City imeshinda mechi yake ya kwanza dhidi ya AS Roma ya Italia kwa mikwaju ya penati 5 kwa 4 baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2… magoli yaliofungwa na Raheem Sterling dakika ya 3 na Kelechi Iheanacho dakika ya 51 kwa upande wa Man City huku yale ya AS Roma yakifungwa na Miralem Pjanic dakika ya 8 na Adem Ljajic 87.
Huu pia ni mchezo wa kwanza kwa Raheem Sterling toka ajiunge na klabu ya Man City akitokea Liverpool kwa dau la pound milioni 49.
Nimekusogezea picha na video za magoli mtu wangu.
Hapa kuna video zinazoonesha magoli yote yalivyofungwa.
Penalti zote hizi hapa
No comments:
Post a Comment