22 July, 2015

Victoria Kimani aibua mjadala mkali hasa baada ya mashabiki wengi kuweka wazi hisia zao dhidi yake

Star wa muziki Victoria Kimani wa nchini Kenya, amekuwa kivutio cha mjadala mkubwa katika mtandao wa twitter, hasa baada ya mashabiki wengi kuweka wazi hisia zao dhidi ya diva huyo.

Baadhi yao wameelezea kuwa, msanii huyo amekuwa si mzalendo na mwenye uwezo mdogo, akibebwa na sapoti ya usimamizi mzuri wa muziki wake.

Majadiliano hayo yamezuka baada ya mwanadada huyo kutoa lawama zake kuwa wakenya wamekuwa na uzalendo mdogo katika kuwasapoti wasanii wao kuweza kufanya vizuri nje ya nchi, binafsi akionekana kuwa mbali na nchi yake, akiwa anasimamiwa na lebo kutoka Nigeria.

Hata hivyo, staa huyo hajaonesha kurudishwa nyuma na matani mengi ya mashabiki kuhusu muziki wake huo, na kuwashukuru wote walioshiriki kutoa maoni yao kuhusu yeye wakitumia trend ya #someonetellVictoriakimani.





No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...