Kuna video moja imeonekana leo ikimuonesha Straika wa Napoli, Gonzalo Higuain akizinguana na watu mjini Ibiza, Hispania.
Kwa mujibu wa ripoti, video hiyo ilirekodiwa alfajiri ya leo
wakati nyota huyo mwenye miaka 27 akiondoka katika klabu moja ya usiku
inayojulikana kwa jina la Pacha iliyopo kisiwani humo.
Higuain alikuwa anakula bata na mshambuliaji wa PSG, Ezequiel Lavezzi katika klabu hiyo, wanaripoti El Mundo.
Baada ya mshambuliaji huyo kuamua kurudi nyumbani, alizingirwa
na mashabiki ambao walitaka asaini autograph, lakini Higuain alikataa na
kuanza kuzinguana nao mpaka kufikia hatua ya kutaka kupigana.
Higuain alishikwa na mlinzi wake, na alipogundua tuko lile limerikodiwa alifoka kwa sauti:
“Futa video vinginevyo nitakupasua kichwa”.
Hata hivyo tukio hilo halikuendelea….Tazama video hapa chini:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment