Wimbo mpya umetolewa nchini Uganda mwimbaji akiwa rais wa Uganda Yoweri
Museveni . Lakini bado bado haijafahamika wazi ikiwa yeye binafsi ndie
aliyeutoa ama alishiriki katika kuutoa.
Hata hivyo kuna tetesi kwamba ni wimbo mpya wa kampeni za uchaguzi mkuu
ujao 2016. Sauti bila shaka ni rais Museveni, wimbo unaitwa Yegoma.
Maana yake kwa taji --- kama la ufalme.
Maneno ya wimbo yanelezea uchungaji wa ngombe , ala za muziki na maisha marefu.
Beti ya kwanza inasema (Oruyogo-yongo - orwa Kabale) ikimaanisha
usisalimu amri. Katika picha ya Video ya wimbo huo inaonyesha ndege aina
ya Kulastara akijaribu kummeza chura, lakini chura anamkaba ndege
kooni. Oruyongoyongo ni ndege anayekula nyoka na panya.
Na katika ubeti wa mwisho Rais anazungumzia maisha marefu na kuwaambia
wasikilizaji kwamba wimbo kama Yengoma na Mpenkoni zinatakiwa kubaki
katika jamii wakimukumbuka. Wimbo wa ''Mpenkoni'' yaani nipe fimbo,
ulitumiwa na katika kampeni bwana Museveni ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2011.
Wimbo huu mpya umetolewa ikiwa rais Yoweri Museveni anakabiliwa na upinzania mkubwa katika chama chake tawala cha NRM.
Aliyekuwa waziri wake mkuu Amama Mbabazi na makamu wake wa zamani
Prof.Gilbert Bukenya wametangaza nia ya kugombea kiti cha urais kwa
chama tawala anachokiongoza rais Museveni.

No comments:
Post a Comment