Tetesi za usajili wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Angel
Di Maria kuondoka Old Trafford na kujiunga na Paris Saint Germain leo
zimechukua sura mpya.

Kwa
siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa vimekuwa
vikiripoti kwamba mchezaji huyo angeuzwa kwa ada ya zaidi ya Euro
Millioni 60 na angetambulishwa rasmi na PSG Ijumaa hii, lakini kwa
mujibu wa kituo cha Televisheni cha BeIN Sports kinachomilikiwa na bwana
Nasser Ghanim Al-Khelaifi, ambaye mmiliki wa klabu ya PSG – ni kwamba
klabu hiyo imeghairi kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo baina ya
United na PSG yameisha rasmi.

Akiwa na miaka 27, Manchester United walivunja rekodi ya usajili ya
Uingereza kwa kulipa kiasi cha £59.7m kumsajili Angel Di Maria lakini
muargentina huyo ameshindwa kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu ya EPL na
inaaminika anavutiwa na wazo la kwenda PSG.
Hata hivyo, inaonekana vilabu hivyo vimeshindwa kuafikiana juu, huku
CEO wa United akiripotiwa kutaka kurudisha fedha zote walizotumia
kumpata winga huyo.
No comments:
Post a Comment