25 October, 2016

Sipendi 'bifu' na msanii yeyote - Joh Makini

Msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Joh Makini amesema katika vitu ambavyo hapendi kwenye kazi zake za kisanii ni kuwa na 'bifu' na msanii mwenzake katika tasnia ya sanaa nchini.
Makini ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva waliokusanyika kushuhudia program maalumu ya Kamatia Kitaa katika  kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
“Sipendi kuwa na bifu na msanii yeyote , mimi naamini katika muziki wangu na kuheshimu kila mmoja katika kazi yake” Amesema Makini
Aidha Makini ameongeza kuwa katika mambo ambayo humuumiza sana ni kuona kazi za wasanii zikiwa zimezagaa mtaani na kuuzwa bila wasanii kunufaika na chochote.
“Jambo hili inabidi serikali iingilie kati kwa sababu ugumu wa maisha mtaani umefanya vijana kuanza  kudurufu kazi zetu na kuziuza bila sisi kunufaika na chochote na jambo hili linatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha “ Amesema Joh Makini.

Pamoja na hayo Makini amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwani kundi la weusi limejipanga vyema katika kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki.

CHANZO: eatv.tv

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...