Nguli wa muziki nchini Afrika
Kusini, Mduduzi Tshabalala, al-maarufu Mandoza, amefariki baada ya
kuugua saratani kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 38.Mandoza alisifika kwa albamu kadha za muziki aina ya Kwaito, aina ya muziki wa Afrika Kusini ambao hukaribiana sana na Hip Hop.Nyimbo zake nyingi sana zilivuma, zikiwemo nyimbo kutoka albamu yake ya kwanza Nkalkatha. Familia ya Mandoza imesema mwanamuziki huyo aligunduliwa kuwa na saratani baada ya kuanza kuumwa na kichwa sana pamoja na kutatizwa na macho mwaka mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment