Justin Bieber aliondoka katika
jukwaa la tamasha yake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki
kutopiga kelele wakati anapoimba.
Na mashabiki hao walipokataa kusitisha kelele zao aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa,huku baadhi ya mashabiki wakimzoma.
Baadaye kijana huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha yake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.
''Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho ,munajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana''.
No comments:
Post a Comment