KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthibitisha manunuzi yake.
Taarifa iliyotolewa jana na SEEA ilisema urejeshaji wa fedha baada ya kuthibitika kwa manunuzi ni moja ya njia mbili za nafuu kwa wateja wa Samsung Note 7.
Mbali na urejeshaji fedha, SEEA imesema katika taarifa yake, wateja wenye simu za Samsung Note 7 wanaweza pia kuamua kuzibadilisha na kupatiwa simu mpya za Galaxy S7 au Galaxy S7 Edge, au Galaxy Note 5, pamoja na chenji itokanayo na tofauti ya bei.
SEEA imesema katika taarifa yake kuwa inafahamu kwamba simu za Note 7 zilikuwa hazijaanza kuuzwa katika soko la nyumbani, lakini kwa kuwa imeweka mbele usalama wa wateja wake ipo tayari kuchukua jukumu hilo.
Note 7 zimegundulika kuwa na tatizo katika betri ya simu hiyo ambayo husababisha kulipuka, lakini hata baada ya kubadilishwa baadhi ya wateja waliopata simu za toleo la pili pia wameelezea kuwapo kwa tatizo hilo pia.
SEEA imesema ofa yake ni kwa wateja wa aina zote mbili, walionunua mara ya kwanza katika msoko nje ya Afrika Mashariki na wanaomiliki Note 7 baada ya kubadilishiwa walizonunua mara ya kwanza.
26 October, 2016
Video mpya ya Taylor Gang Ft Wiz Khalifa na Tuki Carter ‘Sleep At Night’.
Wiz Khalifa na kundi lake la Taylor Gang wametoa video ya wimbo wao mpya “Sleep at Night” kutoka kwenye album ya TGOD Volume 1. yenye nyimbo 23 ikiwa na wasanii kama Ty Dolla $ign, Juicy J, Berner, Chevy Woods, na Raven Felix.
Aliyekuwa beki wa Brazil Carlos Alberto afariki
Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu
ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi
kilichoshinda kombe la dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa mika
72.
Beki wa kulia Alberto alichezeshwa mara 53 na Brazil na kushinda mataji ya nyumbani dhidi ya Fluminense na Santos ambapo alishiriki mara 400.
Alifariki mjini Rio de Janeiro kufuatia mshtuko wa moyo.
Gambia kujiondoa katika mahakama ya uhalifu ICC
Serikali ya Gambia imesema kuwa itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mara moja.
Hatua hiyo imekuja kutokana na madai kuwa ICC hushughulika na Waafrika pekee.Maamuzi ya kujitoa katika mahakama hiyo yanafuatia baada ya Burundi na Afrika ya Kusini kutangaza kujiondoa
Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh amekua madarakani tangu mapinduzi nchini humo mwaka 1994.
Uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika desemba lakini mapema mwaka huu viongozi nane wa upinzani walikamatwa na kuhumiwa miaka mitatu jela kwa kuhusika katika maandamano ambayo hayakua na kibali.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limesema kuwa maamuzi hayo ni sehemu ya muendelezo wa ukandamizaji wa haki za binadamu nchini Gambia.
Mkongo amvuruga Kadjanito, abadili na dini
Msanii wa Bongo fleva Khadija Said Maige maarufu kama Kadjanito
amefunguka na kusema kuwa amepagawa na mapenzi ya Tresor Lisimo mchezaji
wa mpira ambaye ndiye anataka kufunga naye ndoa tarehe 29 mwezi wa 10
mwaka huu.
Kadjanito kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na kituo cha Tv EATV anasema aliona amekaa peke yake kwa muda mrefu hivyo ameamua kuwa mke wa mtu ili na yeye awe mwanamke aliyekamilika sababu amempata mtu anayependana naye na mtu ambaye wanaelewana.
"Nimeamua kufunga ndoa kwani nilikaa muda mrefu peke yangu nikatafakari nikaona siyo kitu kizuri nikiwa kama msichana ambaye nina 'Inspire' watu wengi lazima kuna vitu nifanye ili niwe mwanamke kamili, maana ukiwa peke yako mtu anaweza kukuchukulia labda huyu mtu muhuni lakini mimi nimeamua kuwa mke wa mtu, najua ni kitu kikubwa lakini haitanifanya mimi niache kazi zangu za muziki"
Ameendelea kusema "Nimeamua kufunga ndoa sababu nimeona nimepata mtu ambaye tunapendana, ninaendana naye na ninampenda sana. Aisee mimi nafunga ndoa ya Kikristu yaani jamaa nimemzimia mpaka nimeamua kumfuata katika imani yake, kiukweli ninamfuata" alisema Kadjanito

25 October, 2016
Mmiliki wa Mtandao wa Wikileaks afariki Dunia
Mwanzilishi wa mtandao maarufu wa Wikileaks, Gavin MacFadyen (76)
amekutwa amefariki Jumamosi ambapo chanzo cha kifo chake bado
hakijajulikana.
Mtandao wa Wikileaks umekuwa ukiibua mambo mbalimbali ya siri ya mgombea urais wa Marekani, Hillary Clinton.
Wengi hawajayaamini kifo chake ambacho kimewastua na kuumiza mioyo ya watu wengi hasa pale wanapomkumbuka marehemu kama mwanzilishi wa kituo cha habari za uchunguzi (Centre for Investigative Journalism) mwaka 2003 ambapo wanahabari wengi wakubwa duniani wamejifunza hapo.

List ya Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji Bora wa Dunia
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza majina ya wachezaji 30
ambao wanataraji kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia kwa mwaka 2016
maarufu kama Ballon d’Or.
Majina ya wachezaji ambao wanawania tuzo hiyo kwa mwaka huu imeongezeka kutoka 23 hadi 30 na Disemba 13 yatatangazwa majina ya wachezaji watatu ambao wataingia katika kinyang’anyiro kwa kupigiwa kura na mshindi kupatikana.
Wachezaji 30 ambao wametajwa kuwania Ballon d’Or 2016 ni kama Ifuatavyo
Sergio Aguero (Manchester City),
Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund),
Gareth Bale (Real Madrid),
Gianluigi Buffon (Juventus),
Cristiano Ronaldo (Real Madrid),
Kevin De Bruyne (Manchester City),
Paulo Dybala (Juventus),
Diego Godin (Atletico Madrid),
Antoine Griezmann (Atletico Madrid),
Gonzalo Higuain (Juventus),
Zlatan Ibrahimovic (Manchester United),
Andres Iniesta (Barcelona),
Koke (Atletico Madrid),
Toni Kroos (Real Madrid),
Robert Lewandowski (Bayern Munich).

Music: PHARRELL – ‘RUNNIN”
Pharrell Williams ameachia ngoma mpya ambayo itatumika katika movie ya Hidden Figures, ndani ya wimbo huo Pharrell amezungumzia juu ya wanawake na haki zao.
New Video: Qboy ft Rayvanny & Shetta – Mugacherere [Official Music Video]
Stylist wa mkali wa Bongo Fleva, Diamond na kutoka kambi ya WCB, Q boy
ameachia video ya single yake mpya ‘Mugacherere’ aliyowashirikisha Ray
Vanny na Shetta.
Pluijm: Mzambia kuinoa Yanga?
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm,amesikitishwa na kitendo cha uongozi wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina, bila kumtaarifu, akisema "huko ni kunivunjia heshima".
Pluijm alisema alipaswa kutaarifiwa na uongozi juu ya jambo lolote kuhusu nafasi yake kazini, lakini cha ajabu anajua kupitia vyombo vya habari.
Aidha, kuhusu uwezekano wa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Pluijm alisema:“Sipendelei sana hiyo kazi. Nataka kufanya kazi na wachezaji kila siku kwa matakwa ya moyo wangu. Ila nitakwenda kuwasikiliza, tunaweza kuafikiana kwa lolote, ikiwamo kubaki kama Mkurugenzi wa Ufundi,” alisema.
Pluijm pia akagusia maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu kesho akisema wachezaji wake wote wapo fiti kuelekea mechi hiyo na hana majeruhi.
Yanga imerejea jana kutoka Mwanza, ilikopita ikitokea Bukoba mkoani Kagera ambako Jumamosi ilishinda 6-2 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa Pluijm na wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh na kumpa nafasi Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
CHANZO: Nipashe
Pluijm alisema alipaswa kutaarifiwa na uongozi juu ya jambo lolote kuhusu nafasi yake kazini, lakini cha ajabu anajua kupitia vyombo vya habari.
“Sijaambiwa chochote. Uongozi umenivunjia heshima sana, kwa klabu kama Yanga hawakupaswa kufanya hivyo,”alisema Pluijm.Pamoja na hayo, Pluijm amesema anasubiri kukutana na uongozi wa klabu kujua mustakabali wake rasmi na baada ya hapo atakuwa na ya kuongea zaidi. “Labda nitachukua hatua ya kupumzika kwanza kabla ya kuamua mustakabali mpya,”alisema.
Aidha, kuhusu uwezekano wa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Pluijm alisema:“Sipendelei sana hiyo kazi. Nataka kufanya kazi na wachezaji kila siku kwa matakwa ya moyo wangu. Ila nitakwenda kuwasikiliza, tunaweza kuafikiana kwa lolote, ikiwamo kubaki kama Mkurugenzi wa Ufundi,” alisema.
Pluijm pia akagusia maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu kesho akisema wachezaji wake wote wapo fiti kuelekea mechi hiyo na hana majeruhi.
Yanga imerejea jana kutoka Mwanza, ilikopita ikitokea Bukoba mkoani Kagera ambako Jumamosi ilishinda 6-2 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa Pluijm na wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh na kumpa nafasi Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
CHANZO: Nipashe
Sipendi 'bifu' na msanii yeyote - Joh Makini
Msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Joh Makini amesema katika vitu
ambavyo hapendi kwenye kazi zake za kisanii ni kuwa na 'bifu' na msanii
mwenzake katika tasnia ya sanaa nchini.
Makini ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva waliokusanyika kushuhudia program maalumu ya Kamatia Kitaa katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
Pamoja na hayo Makini amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwani kundi la weusi limejipanga vyema katika kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki.
CHANZO: eatv.tv
Makini ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva waliokusanyika kushuhudia program maalumu ya Kamatia Kitaa katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
“Sipendi kuwa na bifu na msanii yeyote , mimi naamini katika muziki wangu na kuheshimu kila mmoja katika kazi yake” Amesema MakiniAidha Makini ameongeza kuwa katika mambo ambayo humuumiza sana ni kuona kazi za wasanii zikiwa zimezagaa mtaani na kuuzwa bila wasanii kunufaika na chochote.
“Jambo hili inabidi serikali iingilie kati kwa sababu ugumu wa maisha mtaani umefanya vijana kuanza kudurufu kazi zetu na kuziuza bila sisi kunufaika na chochote na jambo hili linatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha “ Amesema Joh Makini.
Pamoja na hayo Makini amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwani kundi la weusi limejipanga vyema katika kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki.
CHANZO: eatv.tv
Kelele zamuondoa Justin Bieber jukwaani kwa hasira
Justin Bieber aliondoka katika
jukwaa la tamasha yake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki
kutopiga kelele wakati anapoimba.
Na mashabiki hao walipokataa kusitisha kelele zao aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa,huku baadhi ya mashabiki wakimzoma.
Baadaye kijana huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha yake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.
''Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho ,munajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana''.
Utafiti: Betri zinazotumiwa katika simu zina sumu
Zaidi ya gesi 100 zinazoweza
kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni
ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya
smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya.
Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.
Katika utafiti huo mpya,walichunguza betri moja ya kuchaji inayojulikana kama Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka.
''Siku hizi,Betri za Lithium-ion hukuzwa na serikali nyingi duniani kama kawi inayopatikana kwa haraka ili kuviwasha vifaa vyote ikiwemo magari ya kielektroniki hadi simu," alisema Jie Sun, profesa mkuu katika taasisi ya ulinzi ya NBC.
Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa.
Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.
CHANZO: BBC.
24 October, 2016
Beki wa Manchester United Eric Bailly aumia vibaya
Beki wa Manchester United anayetoka
Ivory Coast Eric Bailly alipata jeraha mbaya ya goti wakati wa mechi
ambayo timu yake ililazwa 4-0 na Chelsea Jumapili.
ALiondolewa uwanjani dakika ya 52.
"Nina wasiwasi kwamba ni jeraha mbaya," meneja wa United Jose Mourinho alisema. "Ameumia kwenye goti, eneo lenye kano. Anahisi kwamba ni jeraha mbaya sana."
Bailly alikuwa amechezea United mechi zote walizocheza msimu huu ligini.
Alijiunga nao kutoka klabu ya Villarreal ya Uhispania kwa £30m kabla ya kuanza kwa msimu.
22 October, 2016
Jay Mo amwagia misifa Juma Nature
Msanii Jay Mo amesema ukongwe wa Juma Nature kwenye game ya bongo fleva
ni kitu cha kuthaminiwa sana kwani ameleta mchango mkubwa kwenye muziki
huo mpaka kufikia hapa ulipo.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jay Mo amesema wataendelea kumheshimu Juma Nature kwani vitu ambavyo amevifanya, ndivyo vimesababisha wasanii kama kina Diamond kujulikana kimataifa.
Jay Mo amesema kutokana na aina hiyo ya muziki wa Juma Nature, ndiyo ume'inspire' vijana wengi na kufuata nyayo zake, ikiwemo yeye mwenyewe na kuandika mistari ya wimbo wa stori 3 na Jua na mvua.

“Tutamkumbuka kwa kufanya vitu ambavyo vimewafanya mpaka kina Diamond wakajulikana, muziki anaoimba Juma Nature ni ule muziki wa watu wa chini, amegusa maisha ya watanzania halisi, unajua sisi hata kama tulikuwa tunafanya muziki lakini haikuwa kama ya Juma Nature, kipindi hicho unaenda kweny show ya Juma Nature unakuta watu wanapanga foleni ndefu kukata tiketi, alikuwa anaweka kiingilio cha chini ili kila mtu aweze kuingia, hajajichukulia mi super star na kuvaa ukinondoni au u ilala, muziki wake ulikuwa umelalia maisha ya mtaa na watu wengi, alikuwa mjanja kutarget hawa watu wenye uwezo wa chini kimaisha”, alisema Jay Mo.
Jay Mo amesema kutokana na aina hiyo ya muziki wa Juma Nature, ndiyo ume'inspire' vijana wengi na kufuata nyayo zake, ikiwemo yeye mwenyewe na kuandika mistari ya wimbo wa stori 3 na Jua na mvua.
CHANZO: eatv.tv
Collabo yangu na Jay Dee inakuja - Diamond
Baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa mashabiki waliotamani kuona
Diamond Platnumz na mwanadada Lady Jay Dee wakifanya kazi pamoja, wakali
hao wa bongo fleva huenda wakaja na 'collabo' ya hatari, siku chache
zijazo.
Hatua hiyo inatokana na msanii Diamond kufunguka kuwa hakuna sababu yoyote inayowakwamisha kufanya kazi ya pamoja, isipokuwa muda na ratiba zao kubana.
Dangote ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea ofisi za Kituo cha runinga EATV, na kukutana na maswali mbalimbali ikiwemo sababu za wao kutofanya kazi ya pamoja licha ya mashabiki kuitamani 'collabo yao.
"Siku si nyingi tutafanya kazi pamoja na Jay Dee, kilichotukwamisha ni ratiba zetu, lakini pia nilikuwa sijafikiria hilo, ila sasa kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakiomba kila mara, nitawasiliana naye, na tutafanya kazi ya pamoja muda mfupi ujao, hakuna sababu nyingine tofauti na kubanwa na kazi nyingi, pamoja na ratiba zetu kutoendana"
Kuhusu ni lini mashabiki wategemee kazi hiyo, Dangote alisema kuwa hawezi kuahidi tarehe, lakini ana uhakika 'collabo' hiyo inakuja.
CHANZO:eatv.tv

Twitter na makampuni mengine Marekani yavamiwa na Wadukuzi(Hackers)
Uchunguzi umeanzishwa baada ya
uvamizi wa mitandao kadhaa dhidi ya kampuni ya Marekani ulioathiri
huduma za baadhi ya mitandao hiyo.
Twitter, Spotify, Reddit, Soundcloud na mitandao mingine yameathirika katika uvamizi wa mitandao.Kumekuwa na hofu kuhusu tishio dhidi ya usalama wa mitandao ya Marekani wakati uchaguzi mkuu ukikaribia baada ya wavamizi kufanikiwa kufikia barua pepe za chama cha Democratic na baadhi ya mashirika ya uchaguzi nchini.
Mitandao hiyo ni wateja wa kampuni iitwayo Dyn ambayo inaitumia kuwasaidia wateja kupata mitandao hiyo wakiyatafuta.
DynDNS imeathirika na uvamizi wa data katika kinachojulikana kama shambulio la (DDos) jambo linalofanya kuwa vigumu kwa wateja kuyapata mitandao hiyo wanapoyatafuta.
Haijulikani wazi ni nani anayehusika na uvamizi huo au ni kwanini Dyn imelengwa.
Katika taarifa kwenye mtandao wake, Dyn imesema uvamizi huo wa DDoS ulianza mapema Ijumaa Marekani na kuathiri kampuni zaidi mashariki mwa taifa hilo.
Athari ya awali ya uvamizi huo ulisababisha baadhi ya mitandao kutopatikana wakati watu wakiyatafuta au wakati mwingine agizo linalotumwa katika mtandao kuchukua muda mrefu kabla ya kupokewa.
Watu wengi waliokuwa wanatumia mitandao ya kijamii walieleza kuwa, Reddit, Twitter, Etsy, Github, Soundcloud, Spotify na mitandao mingine ilikuwa vigumu kuyafungua.
Mitandao pia kama Paypal, Pinterest na Tumblr pia yanaarifiwa kuathirika.
Katika ujumbe kwenye Twitter, na uliosambazwa pakubwa, Github ilisema "tukio la kimataifa" linaathiri Dyn na kufanya kuwa vigumu kuyapata mitandao yake.
Athari ya uvamizi huo ulidhihirika kwa saa kadhaa na kufikia mchana Ijumaa, Dyn ilisema huduma zake zimerudi kama kawaida.
Ligi kuu bara leo kuendelea Viwanja sita kuwaka moto
Ligi Kuu ya Tanzania Bara raundi ya 12 inaendeleaLeo(Jumamosi) kwa
michezo sita ambako mabingwa watetezi Young Africans ya Dar es Salaam
itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba
mkoani Kagera.
Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon itakuwa mwenyeji wa Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo utaofanyika Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani – Mvomero.
Majimaji itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea. Michezo yote mitano hapo juu itaanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki lakini mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu itaanza saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam huko Chamazi-Mbagala Dar es Salaam.
Jumapili itakuwa ni zamu ya kinara wa ligi hiyo, Simba ambayo itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Tanzania Prisons itapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

21 October, 2016
Video mpya Tekno ‘Diana’ itizame hapa
Kutoka Nigeria ni hit maker wa Duro, Pana na ngoma nyingi sii mwingine bali ni Tekno na hii ni video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la Diana. Itizame hapa kwa kubofya Play hapo chini.
New Audio Single sally Ft. Godzila – IWanna Know Mp3 Download
Single sally msanii kutokea pande za Moshi ambaye anafanya poa katika game as an upcoming artist na hii ni Track yake inayokwenda kwa jina la IWanna Know akiwa kamshirikisha mkali Godzila a.k.a King Zila. Download ngoma hiyo kwa kubofya DOWNLOAD hapo chini.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
Mpenzi msomaji wa safu hii ni siku nyingine tunakutana katika kujuzana,kukumbushana, na kuelimishana mila na desturi za makabila mbalimbal...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
-
This is a song sang by a very gifted woman Adele, I sang it to show world that everyone appreciate and love to enjoy good music! Asa...