Zaidi ya gesi 100 zinazoweza
kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni
ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya
smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya.
Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.
Katika utafiti huo mpya,walichunguza betri moja ya kuchaji inayojulikana kama Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka.
''Siku hizi,Betri za Lithium-ion hukuzwa na serikali nyingi duniani kama kawi inayopatikana kwa haraka ili kuviwasha vifaa vyote ikiwemo magari ya kielektroniki hadi simu," alisema Jie Sun, profesa mkuu katika taasisi ya ulinzi ya NBC.
Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa.
Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.
CHANZO: BBC.
No comments:
Post a Comment