Beki wa Manchester United anayetoka
Ivory Coast Eric Bailly alipata jeraha mbaya ya goti wakati wa mechi
ambayo timu yake ililazwa 4-0 na Chelsea Jumapili.
ALiondolewa uwanjani dakika ya 52.
"Nina wasiwasi kwamba ni jeraha mbaya," meneja wa United Jose Mourinho alisema. "Ameumia kwenye goti, eneo lenye kano. Anahisi kwamba ni jeraha mbaya sana."
Bailly alikuwa amechezea United mechi zote walizocheza msimu huu ligini.
Alijiunga nao kutoka klabu ya Villarreal ya Uhispania kwa £30m kabla ya kuanza kwa msimu.
No comments:
Post a Comment