Serikali ya Gambia imesema kuwa itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mara moja.
Hatua hiyo imekuja kutokana na madai kuwa ICC hushughulika na Waafrika pekee.Maamuzi ya kujitoa katika mahakama hiyo yanafuatia baada ya Burundi na Afrika ya Kusini kutangaza kujiondoa
Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh amekua madarakani tangu mapinduzi nchini humo mwaka 1994.
Uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika desemba lakini mapema mwaka huu viongozi nane wa upinzani walikamatwa na kuhumiwa miaka mitatu jela kwa kuhusika katika maandamano ambayo hayakua na kibali.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limesema kuwa maamuzi hayo ni sehemu ya muendelezo wa ukandamizaji wa haki za binadamu nchini Gambia.
No comments:
Post a Comment