Pluijm alisema alipaswa kutaarifiwa na uongozi juu ya jambo lolote kuhusu nafasi yake kazini, lakini cha ajabu anajua kupitia vyombo vya habari.
“Sijaambiwa chochote. Uongozi umenivunjia heshima sana, kwa klabu kama Yanga hawakupaswa kufanya hivyo,”alisema Pluijm.Pamoja na hayo, Pluijm amesema anasubiri kukutana na uongozi wa klabu kujua mustakabali wake rasmi na baada ya hapo atakuwa na ya kuongea zaidi. “Labda nitachukua hatua ya kupumzika kwanza kabla ya kuamua mustakabali mpya,”alisema.
Aidha, kuhusu uwezekano wa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Pluijm alisema:“Sipendelei sana hiyo kazi. Nataka kufanya kazi na wachezaji kila siku kwa matakwa ya moyo wangu. Ila nitakwenda kuwasikiliza, tunaweza kuafikiana kwa lolote, ikiwamo kubaki kama Mkurugenzi wa Ufundi,” alisema.
Pluijm pia akagusia maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu kesho akisema wachezaji wake wote wapo fiti kuelekea mechi hiyo na hana majeruhi.
Yanga imerejea jana kutoka Mwanza, ilikopita ikitokea Bukoba mkoani Kagera ambako Jumamosi ilishinda 6-2 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa Pluijm na wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh na kumpa nafasi Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.
CHANZO: Nipashe
No comments:
Post a Comment