Kiongozi wa chama cha upinzani cha
Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda, Kizza Besigye
amekamatwa pamoja na wanachama wengine wa chama chake.
Kukamatwa
kwao kunajiri wakati ambapo chama hicho kilikuwa kinaanza kampeni zake
kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kulingana na mwandishi wa BBC Patience
Atuhaire katika mji mkuu wa Kampala.Watu wengine wawili pia walikamatwa pamoja na bwana Besigye wakati maafisa wa polisi walipovamia nyumba yake mapema leo kulingana na vyombo vya habari.
Mbunge wa chama hicho Ssemujju Nganda ambaye pia ni msemaji wa chama hicho pia alikamatwa nyumbani kwake na amepelekwa katika kituo cha polisi cha Naggalama,karibu na mji mkuu wa Kampala.
Besigye amepoteza mara tatu kwa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi uliokumbwa na utata.
No comments:
Post a Comment