CEO kutoka kwenye lebo ya Hustle Gang T.I ameingia kwenye headlines baada interview yake na Dj Whoo Kid kwenye moja ya radio nchini Marekani… akiwa kwenye interview hiyo T.I alizungumzia mipango yake ya kufanya collabo na Usher Raymond, Young Thug na B.O.B pia alizungumzia changamoto alizokumbana nazo kwenye kufanya kazi na rapper Travis Scott.
Baada ya kutumia dakika 12 kuongelea vitu vyote hivyo T.I akaulizwa swali linalohusiana na hali ya Siasa sasa hivi nchini Marekani haswa wagombea nafasi ya Urais nchini humo wakiwemo Donald Trump na Hillary Clinton ambae mume wake Bill Clinton alishawahi kuwa Rais wa Marekani pia…
>>> ”
Sio kwamba nina ubaguzi wa kijinsia ama nini ila kusema kweli siwezi
kumchagua mwanamke kuwa kiongozi wa nchi ya Marekani… kwa sababu nawajua
wanawake na mara nyingi wanafanya maamuzi yasiokuwa ya msingi kwa
kufuata mioyo na hisia zao. Huwa wanafanya maamuzi ya mambo mazito kwa
vile wanavyojisikia wakati huo alafu badaae wanasema hawakudhamiria
kufanya maamuzi hayo… nisingependa kumchagua mwanamke alafu aje kufanya
haya..” <<< T.I.
Baada ya interview hii T.I alishambuliwa na watu mbalimbali wengi wakimuuita mbaguzi wa jinsia, wengine wakisema anachukia wanawake… kila mtu alisema lake!
No comments:
Post a Comment