14 October, 2015

Je, unayafahamu haya kuhusu wanawake?


Kuna usemi mmoja nimezoea sana kuusikia “I can’t understand women” hii ni nyimbo kila mwanaume anaimba, inawezekana ikawa kweli, kutokumuelewa mwanamke, inawezekana ikawa inasababishwa na wewe kutokuelewa mambo kadhaa yanayowahusu wanawake, hapa tafiti wa  kisayansi  na zisizo za kisayansi  zitakusaidia kumuelewa mwanamke kisaikologia na kitabia.
  1. Mapigo ya moyo ya mwanamke hupiga haraka kuliko mwanaume.
Maumbo ya wanawake huwa si makubwa kama ya wanaume , kwahiyo mioyo yao huwa inapiga mara nyingi, moyo wa mwanamke unapiga mapigo 78 ndani ya dakika moja.

  1. Mwanamke anaongea maneno 20,000 kwa siku wakati mwanaume anaongea maneno 13,000 tu kwa siku. Inawezekana ni watu wa maneno mengi na stori nyingi pia.

  1. Mwanamke hulia mara 30-64 kwa mwaka. Inasemekana tatizo la homoni, kuna asilimia 60% ya homoni inayoitwa prolaktini kwa wanawake kuliko kwa wanaume

  1. Mtaalamu wa Kwanza wa Program za Kompyuta (computer programmer) ni Mwanamke. Nani kasema wanawake hawawezi hesabu , Ada Lovelace (1815 -1852 ) ndio mwanamama  wa kwanza kufanya program za kompyuta.  Na inasemekana  katika rekodi zilizowahi kuwekwa  mtu wa kwanza kugundulika kuwa na  Uwezo mkubwa wa kufikiri (IQ)  ni Mwanamke.

  1. Wanawake wanapenda sana Chokoleti kuliko Tendo la ndoa. Utafiti unaonyesha wanaume wanapenda sana kufanya mapenzi kuliko wanawake, wanaume hutumia sana akili wakati wanawake ni watu wahisia zaidi,(emotions) hisia gani wanazipata wanawake wakila chokoleti hilo ni kwa wanaume kujiuliza.

  1. Asilimia 30 tu ya wanawake huwa wana furahia tendo la ndoa, wanawake wengi huwa hawatimiziwi haja zao za mwili na wengi wao hudanganya kama wameridhika, ila ukweli ni kwamba wachache kufikia haja zao kikamilifu. Inaweza ikawa ni matatizo ya kisaikologia au wanaume kutokujua wapenzi wao wanaridhika na nini.

  1. Kila mwanamke ana kitu kimoja hapendi juu ya mwili wake. Inaweza ikawa ni ukubwa wa matiti yake, tumbo lake au miguu yake hii inategemaa na mtu na mtu

  1. Akili ya mwanamke ni safi kuliko ya mwanaume, hii ni kwasababu mwanamke ni mtu wa vitu vingi akili ya mwanamke inaweza kuwa safi mara nyingi kuliko wanaume, akili chafu au wanaita Dirty mind hii ni kwa wanaume zaidi.

  1. Wanawake wana uwezo mkubwa wa kusikilizaa, wanaume wanasikiliza na upande mmoja tu wa ubongo,upande wa kushoto wa ubongo wao katika kusikiliza wakati wanawake wanatumia pande zote mbili katika kusikiliza .

  1. Wanawake wanaishi miaka mingi kuliko wanaume Dunia . Hii inaweza kuelezwa na sababu mbalimbali , kiwango cha homoni (Testosterone na estrogen) wanawake wana  uwezo mkubwa wa kuzoea mazingira kuliko wanaume . Hata hivyo, kuwa na muda mrefu wa kuishi haina maana wanawake wana  afya bora  kuliko wanaume.  Ila mazingira ambayo wanaume wanaweza yakawashinda wanawake wanayaweza.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...