15 October, 2015

Ulishawahi kujiuliza kuna maneno gani mengine ya kumwambia mpenzi wako tofauti na ‘I love you’ ?


‘Nakupenda’ ni  neno tamu ambalo unaweza mwambia  hivyo  mpenzi wako mara kwa mara lakini si neno pekee ambalo watu wengi wanapenda kusikia mara kwa mara. Yapo mambo mengi ya kumwambia mpenzi wako apate amani, hii inajenga upendo na  Heshima kati yenu.
  1. Mwambie Anaweza:
Kuna wakati tunapitia mambo magumu sana katika maisha na watu wanakata tamaa ya maisha wanakosa uthubutu wa kujaribu tena na tena, kama amefeli mtihani,amepata ajari ya gari, amepata hasara ya kibiashara mwambie “baby you can” mwambie anaweza kuendelea na maisha yataendeleea mtie moyo hii itamfanya ajiamini na kuona thamani yake kwako.

  1. Unanivutia
Mwambie ni kiasi gani anakuvutia, mwambie alivyo mrembo/mtanashati  mueleze ni kiasi gani unakuwa  na furaha akiwa karibu nawe, hii itamsaidia mpenzi wako kujiamini.  Msifie mpenzi wako  kwa suti au tai yake mpya , msifie msichana  kwa kiatu chake na gauni lake zuri kabla hajatoka nyumbani sababu anaweza akasifiwa na wengine, kwahiyo kuwa wa kwanza kumpa sifa hizo atajisikia wa fahari.

  1. Unajivunia kuwa Nae
Mambo yanaweza yasiwe vile mnavyotaka wakati wote, kuwa karibu na mwenza wako  na umuelezee ni kwa kiasi gani unajivunia kuwa nae, nafasi yake katika maisha yako na umuhimu wake ni faraja kwako, mueleze na umuonyeshe pia matendo yanaongea zaidi ya maneno.  Mwambie “am proud of you”

  1. Omba Kutoka Nae.
“Let’s go out”  hapa wasichana wengi huwa wanasubiri watoke na wapenzi wao mpaka waambiwe au mpaka mpenzi wake apange kutoka nae, chukua nafasi ya kumtoa  mpenzi wako mara moja moja na ugharamie huduma zote za siku hiyo, kama ni safari ufukweni, hotelini au migahawa mjini. Kama msichana kuwa tofauti na wale wasichana wanaosubiri kila siku ofa za mpenzi, kuwa tofauti usisubiri mpenzi wako akutoe, mtoe wewe siku moja.

  1. Msamaha
Uwe mwepesi wa kusema neno samahani kila mara, kuna kukoseana mara kwa mara kuwa wa kwanza kuomba msahama hii itapunguza hasira za mapenzi wako na malumbano pia hayatapata nafasi, hii itasaidia kuhimarisha mahusiano ya muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...