15 October, 2015

Lil wayne ajichanganya baada ya Lamar Odom kuzidiwa, aandika ‘R.I.P’

Mchezaji wa zamani wa timu ya kikapu ‘LA Lakers’ na mume wa zamani wa Khole kardashian, Lamar Odom yupo hoi kitandani baada ya kudaiwa kutumia kiwango kikubwa cha dawa za kulevya Cocain kiasi cha kupaatwa na kiharusi na figo zake kushindwa kufanya kazi.Lil wayne ni mmoja ya mastaa wakubwa waliopokea habari hiyo tofauti na ukweli halisi, alitweet “R.I.P LO,Dam man. My blessings to ur fam and friends.” lakini baada ya muda aligindua kuwa alikua amejichanganya, na kuwa mcheza kikapu huyo bado yupo hai, Alitweet tena  “Woop.”

Vyanzo mbalimbali vimedai kuwa Odom aliamua kubwia unga kwa kiasi kikubwa baada ya kupokea simu iliyomuudhi inayohusiana uhusika wake kwenye show ya Keeping up with the Kardashians hata hivyo wanafamilia hao wa The kardashians walifika Hospitalini hapo kumjulia hali.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...