Aliyekuwa mchezaji wa mpira wa vikapu nchini Marekani Lamar Odom
anatibiwa hospitalini baada ya kupatikana amezirai katika danguro mjini
Nevada ,kulingana na mamlaka. Maafisa wa polisi waliitwa katika danguro
la Love Ranch huko Crystal mjini Nevada baada ya kupatikana akiwa hana
fahamu siku ya jumanne.
M'marekani huyo alibebwa na gari na kupelekwa hadi hospitalini kwa kuwa
alikuwa mrefu mno kubebwa katika ndege. Bwana Odom mwenye umri wa miaka
35 amezichezea Miami,Dallas na Los Angeles Lakers pamoja na Clippers.
Pia aliichezea Marekani katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2004 na kushinda medali ya shaba.
Ugonjwa wake haujulikani lakini wasamaria wema walituma ujumbe wao kwa mtandao wa twitter baada ya habari hizo kusambaa.
Bwana Odom ambaye alikuwa amemuoa nyota wa kipindi cha Keeping up with
the Kardashians, Khloe Kardashian amekuwa mnywaji mkubwa wa pombe na
dawa za kulevya.
Alihusishwa na kuendesha gari akiwa mlevi mwaka 2013 na kupigwa marufuku
katika shirikisho la mchezo wa mpira wa vikapu nchini Marekani NBA kwa
kukiuka sheria dhidi ya dawa za kulevya ya mwaka 2000.
Odom na Kardashian waliowana mwaka 2009 katika sherehe ambayo ilionyeshwa katika kipindi cha runinga ya Marekani E.
Walitalakiana mwaka 2013.Odom alishinda ubingwa wa NBA akiwa na klabu ya
Lakers mwaka 2009 na 2010 na alitajwa kuwa mchezaji wa sita bora mwaka
2011. Mara ya mwisho kucheza katika NBA ni mwaka 2013 alipokuwa
akiichezea Clippers.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment