14 October, 2015

KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA



      Kwanza nipende kukusalimu ewe mtanzania mwenzangu kwa kwakusema uu hali gani? Ni matumaini yangu yakwamba uu mzuima na buheri wa afya ingawaje sii asilimia mia moja ni jambo lakumshukuru  MUNGU kwani hapa tulipo sii kwa akili zetu wala kwa ujanja wetu bali ni kwa neema tuu.
       Basi kwa kuyasema hayo ambayo ni salamu zangu kwako wewe mtoka mbali , twende moja kwa moja kwenye mada yetu ambayo teyari nimeiwasilisha kupitia kichwa cha habari hapo juu yakwamba KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA.
   Ni wazi kwamba neno MAISHA sii neno geni masikioni mwetu yakwamba kila mmoja wetu amekua akihangaika hapa na pale, usiku na mchana hii yote ni sababu ya maisha. Nuliwahi kumsikia mzazi mmoja akimweleza mwanae yakwamba ” Mwanangu kuwa uyaone” name nikajiuliza, Je akue ayaone nini? Magari au majumba? Kumbe alikua akimaanisha  MAISHA.
     Maisha ya kijana Mtanzania wa leo yamekua kama kitendawili ambacho kimekosa mtu wakukitegua. Je tumpe nani mji ili aweze Kukitegua?  Yapo mamba mengi yanayo sababisha maisha kuwa magumu au yasiyo na mwelekeo kwa vijana walio wengi na mambo hayo yanatokana na vijana wenyewe na mifumo mibovu ya elimu wapewazo nijana hawa huko mashuleni hasa hasa katika shule za msingi na zile za sekondari.
Kijana mwenyewe anawezaje kuyaharibu maisha yake?
   Yapo mambo mengi mno ambayo kijana akishindwa kuyazingatia wakati wa makuzi yake yanampelekea kija moja kwa moja kupoteza mwelekeo wake katika masha. Mambo hayo ni kama vile : kuto kuweka malengo sahihi katika maisha, Kufuata mkumbo,  tamaa mbaya,  na mtazamo hasi tuliyo nayo vichwani mwetu.  Hayo ni mambo baadhi ambayo kijana mwenyewe anaweza kujisabishia maisha yake kuharibika.
    Kutokuwa na malengo. Kati ya makosa makuu ambayo vijana wengi wanafanya ni kutokuwa na malengo katika maisha yao, na ni wazi yakwamba vijana wengi tumejikuta hatuna malengo sahihi katika maisha yetu ya kila siku, unakutana kijana mtaani amekaa magengeni kwanzia mwanzo wa siku hadi mwisho wa siku hana lolote. Kuwa na malengo ni jambo muhimu mno katiaka maisha ya kila mwanadamu na tambua yakwamba kila aliefanikiwa katika maisha alijiwekea malengo thabiti na akayafuatilia vilivyo kuhakikisha yanatimia. Kumbuka yakua malengo yanendana na ndoto ulizo nazo wewe kama kijana. Ili ndoto yako itimia ni lazima uwe na malengo. Sasa pale kijana anaposhindwa kuwa na malengo ya kweli ndipo anapojikuta akihangaika huku na kule bila mafanikio yeyote.  Ikumbukwe kuwa maisha ni vile unavyoishi  na wewe mwenyewe ndiye utakae hamua yakua maisha yako yawe mazuri au mabala “hatma ya maisha yako ipo mikononi mwako kijana”.
   Labda ni kwa nini kijana anashindwa kuwa na malengo hai katika maisha?
Mara nyingi kijana anakua na tamaa na vishawishi visivyokua na maana. Kama nlivyosema malengo yanawekwa kutokana na ndoto alizo nazo kijana sasa kama huna ndoto na msimamo yakwamba usimamie nini hasa katika maisha ili aweze kujikwamua katika hali ngumu yaki maisha. Tama za hapa na pale na kufuata mkumbo ni vitu ambavyo hupoteza ndoto za vijana wengi, inafika pahala kijana anakuwa anatamaini vitu vingine ambavyo vipo njee ya uwezo wake na kumpelekea kuachana na ndoto zake za mwanzoni na kujiingiza katika vitendo viovu ili kuvipata vitu hivyo.
Kutokuweza kufahamu thamani ya muda; Nipende kuchukua nukuu ya mtu mmoja aliye kuwa maarufu duniani kwa kupitia filamu na huyu sii mwingine ni BRUCE-LEE ambae aliwahi kusema “if you truly love life never play with time coz there is your life originate” vijana wengi tumekuwa tukijikuta tukipoteza muda katika mambo yasiyokuwa na tija katika maisha yetu. Jiulize huko kwenye mitandao yakijamii unapokuwa muda wote huo unafaidika vipi?  Ndio  yawezekana kuna kitu unafaidika nacho lakini kiuhalisia jambo hilo halikusaidii kukukwamua huko ulipo kama unvyotarajia. Kati ya mali tulizo nazo hapa duniani moja wapo ni Muda. Muda ukiutumia vizuri hakika utafanikisha malengo kwa wakati unao taka wewe lakini pindi ukiutumia vibaya hakika utajuta kwan muda ukisha kwenda haurudi nyuma kamwe.  Sasa nacho taka kusema hapa ni kwamba muda sio rafiki ndugu yangu.
    Kutokujiami kama tunaweza peke yetu: katika swala lakujiamini, nimekua nikiliona katika vijana tulio wengi yakua tunakua tukishindwa kujiamini kama peke yetu hatuwezi kabisa. Nipende kuwaambia vijana wenzangu kua tukiishi katika misingi yakutokujiamini tutakua tumeshindwa nakuanguka kimaisha. Unakuta mtu ana fursa katika jamii lakini kijana huyo anaogopa kuichukua fursa ile nauifanyia kazi ili iweze kumwokoa hapo alipo. Watu maarufu duniani waliziona fursa kati yao na wakajaribu na hatimae wakafikia kilele cha mafanikio. Ondoa dhana ya uoga na thubutu kufanya na nakuhakikishia utafikia lengo lango. Acha kujiona huna nguvu wala akili na ukifanya watu watakuonaje. We unadhani Mwalimu JK Nyerere angekua na uoga mbele ya wakoloni leo hii tungekua wapi? Ni mfano tuu ambao tunautoa kutoka kwa baba wa taifa Mwalimu JK Nyerere kwani aliionoa fursa yakudai uhuru wa Tanganyika ndipo akajaribu bila uoga na mwisho wa siku leo hii Tanzania tunatembea vifua mbele.
      Kukataa shule; Niliwahi kuulizwa swali na Mtu mmoja swali ambalo liliniumiza kichwa wakati nlipokua natafuta jibu lake na swali hilo ni “do you think education is certificate in your life?” nikuachie nami hili swali ujibu mwenyewe lakini sintokupatia jibu nlililomjibu mtu Yule. Nipende kuambia kijana mwenzangu ambaye una kataa shule katika dunia ya leo tuna kufananisha na kipofu. Leo hii nani atakuajiri kama hauna elimu? Ndio unaweza kwa namna moja ama nyingine ukajiajiri lakini ukweli ni kwamba hata kujiari kunahitaji elimu. Ubongo wa mwanadamu una ujazo wa lita moja na nusu lakini kalamu na karatasi vina weza kuujaza ubongo huo kwa muda mchache mmno. Nakushangaa sana kwani hata maandiko ya MUNGU yametuambia “mshike sana elimu usimwache aende zake maana yeye ndiye mkombozi wa maisha yako”  ni maandiko yakutoka katika vitabu takatifu na sio maneno yangu mimi Mtokambali. Nipende kukuambia kijana mwenzangu Elimu iwe msingi wa maendeleo yako wewe kijana.
          Hayo niliyo yasema hapo juu ni baadhi tuu ya  mambo ambayo yanaweza kukufanya wewe kijan kuharibu maisha yako kwa ujumla. Nakuahidi katika mwendelezo wa makala hii katika mfululizo wa makala zetu hapa MTOKA MBALI nitakuelezea mambo zaidi yatakayoweza kukuangusha wewe kijana katika maisha yako na jinsi gani utaweza kujikwamua kaitika hayo mambo na kutoka katika UTUMWA wa fikra.
Nipende kukushukuru wewe ulie chukua muda wako ulio wa thamani na kusoma makala hii. Nina amini umepata kitu hapo. Nikusihi kaa hapa hapa kwa vitu moto moto.

Makala hii imeandikwa na FRANCI S MAWERE Kwa udhamini wa MAWERE MEDIA GROUP  Limited (MMGLtd),Kwa mawasiliano nasi tafadhaili piga simu namba 0767322193, au tutumie  barua pepe  mtokambali2015@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...