Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani
nchini Guinea amejiondoa katika uchaguzi uliofanyika nchini humo
akisema kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa uliotekelezwa na serikali
kulingana na kiongozi wake wa kampeni.
Uamuzi huo wa Cellou Diallo
wa kujiondoa unajiri wakati ambapo matokeo yanaonyesha kwamba rais
Alpha Conde anaongoza kwa wingi wa kura akitafuta kushinda awamu ya pili
ya miaka mitano.Wachunguzi kutoka muungano wa Ulaya wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki licha ya matatizo makubwa ya vifaa.
Matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa mwishoni mwa wiki hii.
No comments:
Post a Comment