15 October, 2015

Kisa cha Santos kutaka Neymar afungiwe miezi 6 hiki hapa

Klabu ya Santos ya Brazil imeripotiwa kutuma maombi FIFA imfungie miezi sita mchezaji wao wa zamani Neymar kwa miezi 6 kama sehemu mambo yao ya kisheria dhidi ya mshambuliaji huyo na klabu yake mpya ya FC Barcelona.
  Kwa mujibu wa Sport, Santos wanahisi kusalitiwa na nahodha wa Brazil ambaye kwa mujibu wao alikiuka mkataba baina yao alipojiunga na Barca mwaka 2013. Pia inasemekana wanataka malipo ya fidia ua kiasi cha €55million katika adhabu ambayo wanataka FIFA itoe.
Haijafahamika lini FIFA itatoa maamuzi katika kesi ya Santos dhidi ya Neymar ya kutaka shirikisho hilo limfungie kwa miezi 6.
  Mashtaka ya Santos’ yanaelezea katika toleo la gazeti la Sport: “Neymar anatuhumiwa na Santos kuvunja kanuni namba 63 ya nidhamu. Katika jalada lao la mashtaka pia Santos wamezungumzka namna mchezaji alivyokosa utii wa sheria za uhamisho za FIFA za namba 17(3) and 17(5).”
Neymar amekanusha kuvunja sheria/kanuni yoyote kama anavyotuhumiwa na waajiri wake wa zamani, akisisitiza alihamia Barcelona mara tu baada ya kukubaliana kimsingi na Santos. Kwa mujibu gazeti la Sport, Neymar ana barua ya kutoka kwa Raisi wa Santia Luis Alvaro de Oliveira ambayp ilikuwa inampa ruhusa ya kuanza kuzungumza na Barcelona.
Santos walitangaza kwamba wangemchukulia hatua mchezaji wao wa zamani, baba yake Neymar na Barcelona mwanzoni mwa mwaka huu, wakiwatuhumu kufanya udanganyifu katika majadiliano ya uhamisho wa Neymar. Santos wanasema Barca walifanya udanganyifu katika malipo halisi ya waliyolipa na waliyoyatangaza.
  Ada waliyoripotiwa kulipa Barcelona mwanzoni kwa ajili ya Neymar ilikuwa €57 million (£42 million), lakini uchunguzi wa baadae ulionyesha bei halisi ni €86.2 million (£63.5 million).
Mpaka sasa Raisi wa zamani wa Barca Sandro Rossell na wa sasa Joseph Maria Bartomeu wana kesi mahakamani juu ya udanganyifu huu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...