Ni zaidi ya mara mbili nasikia Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema
akilalamika kuhusu kufanyiwa fitna na watu kwenye Jimbo lake la Vunjo,
leo katika Kikao cha Bunge Dodoma amepewa nafasi tena.. kawasha kipaza
sauti, kalalamika tena kuhusu anachofanyiwa Jimboni kwake.
“Mimi pale
Jimbo la Vunjo Shule ya Muungano iliungua, nilitoa Mil.21 kwenye mfuko
wangu wa Mbunge ili kusaidia, mbona sioni Wizara mmetenga shilingi
ngapi?”
“Mwisho
akaja Katibu Mkuu wa CCM, na nyie CCM mmeanza kushiriki katika uongo..
Katibu Mkuu badala ya kwenda kuwapa pole kwenye Jimbo langu anasema
‘kila Jimbo lina mfuko wa Mbunge ambao ni Mil. 25 kwa miezi mitatu, kwa
mwaka ni Mil.100, hamuwezi kuwa na Kiongozi ambae ni Mbunge na wakati
huohuo ndie Mwenyekiti wa Mfuko huo, je si atajipendelea?’.. Naomba
niulize Serikali, ni kweli Vunjo tumepata Mil. 400 kama alivyosema
Kinana au mnanipakazia?”
“Kwa nini
mnakuja kwangu mnasema maneno ya uongo nyie CCM? Kwa nini CCM
mnanichangia kama mpira wa kona kule Vunjo? Kwa nini mnajiunga na
Wapinzani kwa kusema maneno ya uongo?”
“Mlizonipa
ni Mil.150 lakini mnaenda Vunjo mnawaambia watu nimechukua Mil. 400,
naomba katika Mil. 400 mtoe hizo Mil.150 mnipe hiyo chenji tena leo hii”
“Kwa nini
mnaenda kusema hivyo jamani mna ajenda gani na mimi? Uongo huu
umenisononesha, na mimi nataka niwaambie CCM kwamba habadilishwi mtu
kule Vunjo. Hizi mbinu zinazotumika kunidhoofisha.. Nataka chenji yangu
nikafanye nayo Kampeni”
Msikilize mwenyewe Mbunge Mrema wakati akilalamikia ishu hiyo leo Bungeni Dodoma.>>>>>
No comments:
Post a Comment