Moise
Katumbi, the governor of the Katanga region of the Democratic Republic
of Congo and president of the TP Mazembe Lubumbashi football club,
arrives for their African Champions league football match against Sewe
Sport on March 23, 2014 at the Robert Champroux stadium in Abidjan. AFP
PHOTO / ISSOUF SANOGO
Rais wa klabu ya Tp Englebert Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo Moise Katumbi Chapwe ametajwa kuwa na mpango wa kuingia kwneye
mbio za kuwania urais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo unaotarajia
kufanyika mwakani.Katumbi ambaye amekuwa gavana wa jimbo la Katanga kwa muda mrefu amekuwa pia rais wa klabu ya Tp Mazembe katika kipindi ambacho klabu hii imekuwa na mafanikio ikiwemo kutwaa ubingwa ligi ya mabingwa barani Afrika mara mbili mfululizo pamoja na kufika hatua ya fainali kwenye michuano ya klabu bingwa ya dunia .
Katumbi mwenyewe hajaweka wazi azma hii lakini vyanzo mbalimbali vya habari ambavyo viko karibu na gavana huyu vimekuwa vikihabarisha kuwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa jamhuri ya kidemokrasi ya kongo Katumbi atatangaza azma yake wazi kwa kila mtu.
Chini ya Moise Katumbi Tp Mazembe imekuwa moja ya klabu bora barani Afrika.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekuwa chini ya Joseph Kabila tangu mwaka 2011 wakati baba yake mzazi Laureant Desire Kabila alipouwawa na ameshinda uchaguzi katika miaka ya 2006 na 2011 huku kukiwa na shutuma za kuvurugwa kwa uchaguzi na ukosefu wa hali ya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Kikatiba Kabila hapaswi kugombea mwakani kwani anapaswa kukaa kwa mihula miwili pekee lakini rais huyo hadi sasa amekaa kimya na hajazungumza chochote hali ambayo imezua mijadala ya dhamira ya rais huyo kutaka kuongoza kwa Mhula wa tatu.
No comments:
Post a Comment