22 April, 2016

ELIMU YA TANZANIA YENYE MFUMO WAKIKOLONI



 Mara nyingi ukimkuta mzazi mtaani akiwa na mwanae hupenda sana kumhusia maswala ya elimu. Ni jambo jema kwa mzazi kumuasa mwanae juu ya elimu ya dunia hii maana hata vitabu vitakatifu vilivyo andika maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema Mkamate sana elimu usimwache aende zake kwa  maana ndie mkombozi wa maisha yako. Haya yote ni mwanzo ama utangulizi wa mada yetu ya leo ambayo nimekwisha itambulisha kwako wewe mdau wangu.
    Tanzania ni moja ya nchi zilizowahi kutawaliwa na waingereza enzi zile za ukoloni na hivyo kuifanya kuwa nchi hii kuwa moja kati ya nchi za jumuia ya madola(common wealth). Kiuhalisia nchi hizi huchukua mfumo wa kiuongozi pamoja na mifumo yakielimu kutoka kwa waingereza. Tanzania ni moja kati ya nchi zinazochukua mfumo huo wa elimu kutoka kwa waingereza tangu miaka ya nyuma ambapo Tanzania ikijulikana kama Tanganyika.
Ni elimu ambayo kwa lugha yakigeni inaitwa formal education na wala sii ile ambayo wazee wetu waliipatia chini ya miti yaani informal eduction.

     Elimu ya Tanzania imekua ikionekana kuyumba kutokana na kuingiliwa na wazimu siasa ambapo kipindi cha miaka ya nyuma, elimu hii ilionekana yenye thamani na iliyodhamiria kuijenga jamii nakubadili ama kukuza uchumi wa nchi yetu kwani elimu hiyo ilijikita katika maendeleo ya jamii kwa ujumla wake. Tizama masomo yaliyo pata kufundishwa kipindi cha nyuma katika shule za msingi na hata ufundishaji wake ni tofauti na wa sasa. Watoto wa Mjini wanasema wamechakachua, yawezekana hayo yanasababishwa na utandawazi lakini bado elimu hii ya sasa hapa kwetu ni taabu tupu kulinganishwa na hapo awali.
 Elimu ya mwanzoni ilikua ikimjengea kijana mazingira yakuweza kujiajiri nakujikomboa mwenyewe katika umaskini na taabu lakini hii ya sasa imekua ni tofauti kwani kwa asilimia kubwa imekuwa ikimjengea mwanafunzi mazingira yukuajiriwa ofisi jambo ambalo limekua ngumu na tatizo kuu hapa nchini mwetu na vijana wengi hubaki bila ajira na kurudi nyuma kimaendeleo binafsi na hata maendeleo ya jamii kwa ujumla.
 
  Vijana wengi ambao hawana ajira wamezidi kuongezeka mitaani ni sababu ya msingi mibovu ya elimu yetu hapa nchini. Kijana anasoma mpaka anahitimu lakini mwisho wa siku anabaki pale pale akiranda randa mitaani na bahasha yenye vyeti kibao akitafuta kazi maofisini. Elimu iliyowahi kutolewa miaka ya nyuma ilikua ikimjenga kijana katika mazingira ambayo pindi kijana atakapokua amehitimu masomo yake unakuta teyari kijana huyo anaweza kufanya kitu pasipo kuajiriwa ofisini nikimaanisha kujiajiri.

    Kiukweli mfumo huu wa elimu tulio nao ni mbovu na naweza kusema umepitwa na wakati kwani ni wazi kwamba unamjenga kijana katika mazingira yakutegemea kuajiriwa maofisini kitu ambacho hakitakiwi.
Kwa upande wa sekondari nako ni majanga matupu kwani vijana wengi hapo ndipo ndoto zao huzima mazima. Kwa elimu yetu ni kwamba mwanafunzi akiwa shule ya msingi masomo yake yote kutoa kiingereza hufundishwa kwa Kiswahili lakini pindi anapofikia kuingia sekondari mfumo wa masomo unabadilika na masomo yote kutoa somo lakiswahili ambalo huendeshwa kwa kiswahi na mengine yote ni kiingereza kitupu. Halii hii inakua kigezo kikubwa kinachomfanya mwanafunzi kushindwa kuendena na mfumo huo nakushindwa kufanya vyema katika masomo hayo. Jambo hili linamfanya mwanafunzi kuishia kukariri pasipo kuelewa ni nini anachokifanya.
 
    Kwa upande mwingine Gharama za elimu hii ni ghali kiasi kwamba wapo baadhi ya watoto wetu kushindwa kuendelea na masomo yao. Jambo hili limekua kama chambo chakuvulia kura katika majukwaa ya siasa. Wanasiasa wengi wamekua wakitamba majukwaani kwamba endapo wakiingia madarakani watatoa elimu hii bure, jambo ambalo kiukweli wananchi wanashawishika kuwapigia kura lakini mwisho wa siku hali inabaki pale pale. Siasa za nchi hii ndio zimeharibu kabisa mfumo wa elimu yetu kiasi kwamba haifai tena katika nchi hii.

Wito wangu kwa serekali na wadau mbali mbali wa elimu hapa nchini ni wakae pamoja na kutafuta suluhisho kamili ambalo litaokoa elimu yetu na kuondoa tatizo hili la ajira kwa vijana. Vijana wapewe elimu wajiajiri na sio kungojea kupata kazi maofisini kitu ambacho hata kwenye nchi zilizoendelea Hakipo



123ContactForm | Report abuse

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...