Kwanza
napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na
dunia na vyote vilivyomo tukiwamo sisi wanadamu, kwa mema mengi mno
anayonitendea na hasa kwa kutujalia uhai hadi leo hii.
Kwa
vyovyote vile bila ya Mwenyezi Mungu kutuwezesha na kututia nguvu sisi wenyewe
hatuwezi, bali hali ilivyo ya kimazingira na kimaumbile tutakwama tu, hata hao
wanaokwenda angani na kufanya wanayoyafanya huko si kwa uwezo wao tu, bali pia
ni kwa mapenzi yake Mola
Nipende
kuchua nafasi hii kukukaribisha katika makala yetu leo Juma
pili tarehe 9 mwaka 2015. Leo nitapenda
kuzungumzia shwala hili la Rasilimali ya Misitu tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Katika hali
ya kawaida ni kwamba Misitu tulionayo inatosha kukidhi mahitaji yetu sote tuliopo karibu na Misitu katika mambo ya uhifadhi wa
wanyama pori, kupata vyanzo vya maji, upatikanaji wa mbao kwa ajili ya ujenzi
na hata kupatikana kwa kuni kwa ajili ya kupikia kwa wale wengi wetu
tunayotumia nishati hii ya kuni.
Misitu ya asili ni matokeo ya kazi nzuri
iliyofanywa na Mwenyezi Mungu tangu alipouumba ulimwengu, ikiwamo sayari hii
tunayoishi sisi wanadamu. Kwa maneno mengine, misitu au maliasili zote
tulizonazo ikiwa ni pamoja na madini, wanyamapori, samaki na viumbe wengine
waishio baharini, ardhi (kwa maana ya udongo), maji (kwa maana ya vijito, mito,
maziwa, mabwawa, bahari na ardhioevu), nishati mafuta na gesi asilia ni zawadi
tuliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Kwa bahati nzuri Tanzania Bara imebahatika
kuwa na eneo kubwa lenye misitu ya asili pamoja na mapori mazuri yenye utajiri
mkubwa wa wanyamapori. Kwa takwimu za mwaka 1998 (ambazo sasa zimeboreshwa na matokeo
ya mradi wa kitaifa wa kupima na kutathmini misitu ya asili), Tanzania ilikuwa
na eneo la misitu ya asili la takribani hekta milioni 33.5.
Kati
ya hizo, hekta milioni 13 ni eneo la misitu lililohifadhiwa kisheria (misitu ya
hifadhi ya Serikali Kuu (Central Government Forest Reserves) takribani misitu
600 na misitu 200 ikimilikiwa na Serikali za Mitaa (Local Authority Forest
Reserves) chini ya halmashauri za wilaya); na zaidi ya hekta milioni 20 ya
misitu ya asili bado haijahifadhiwa na kusimamiwa kisheria.
Kwa
kipindi cha miaka 10 iliyopita, vijiji vichache vimeweza kutenga sehemu ya
misitu katika vijiji vyao na kuitangaza kuwa misitu ya hifadhi ya vijiji yenye
jumla ya hekta zaidi ya milioni saba. Hatua hiyo ni ya kupongezwa maana vijiji
husika sasa vina nguvu ya kisheria kusimamia na kutumia misitu husika ipasavyo
na hatimaye kunufaika na usimamizi huo, kwa kuongozwa na Sheria ya Misitu na
kanuni zake.
Vilevile,
vijiji vinayo fursa ya kujiwekea sheria ndogo ndogo kwa lengo la kuimarisha
zaidi utekelezaji wa shughuli za kulinda msitu kwa faida yao na Taifa kwa
jumla. Pamoja na mafanikio hayo, bado sehemu kubwa ya misitu ya asili ambayo
haijahifadhiwa kisheria inapatikana katika maeneo ya vijiji na haitumiki
ipasavyo kuviletea vijiji maendeleo endelevu.
Miaka
zaidi ya 20 Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa Usimamizi Shirikishi wa
Kutunza na Kuendeleza Misitu nchini (Participatory Forest Management-PFM).
Dhana ya Ushirikishwaji ni mbinu ya uongozi inayowezesha kupata mchango wa
mawazo na ushiriki mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali, hasa katika utekelezaji
wa shughuli za kujiletea maendeleo endelevu kwa kutumia rasilimali za asili
tulizonazo.
Ushirikishwaji
husaidia watu kubadilishana mawazo na kufahamu vizuri nini kinaendelea au
kinatekelezwa kwa faida yao. Hivyo kwa kuwashirikisha wanavijiji katika masuala
yanayohusu maendeleo yao vijijini ni suala muhimu sana na huondoa lawama, pia
huongeza motisha wakati wa kutekeleza jambo lililoamuliwa.
Isitoshe,
ni wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa anawajibika ipasavyo katika kutoa
mawazo na kufikia uamuzi sahihi ili lengo na madhumuni ya mipango ya maendeleo
katika sehemu yao iweze kufanikiwa. Ili wanakijiji au jamii katika ujumla wake
waweze kufanya hivyo, ni lazima waelimishwe vya kutosha na kuwajengea uwezo
(capacity) wa kusimamia na kutumia kwa misingi endelevu rasilimali na fursa
zilizopo ikiwamo misitu ya asili.
Swali lililopo ni je tunafaidika
vyema na hizi faida zitokanazo na misitu tulio nayo?
Zipo faida nyingi
zitokanazo na Misitu hii tuliyo nayo na faida hizo
na kama vile kutumika katika maswala ya ufugaji wa nyuki, hifadhi
za wanyama, upatikanaji wa nishati ya kuni na upatikanaji wa mbao ambazo
tunatumia katiaka maswala ya ujenzi na maendeleo hapa nchini.
Ni ukweli
ulio wazi na usiopingika ya kwamba rasilimali hii haitufaidishi ipasavyo na
nathibitisha ukweli huu kwa kutumia mfano mdogo tuu wa upungufu wa MADAWATI mashuleni
mwetu hasa zile za msingi. Kimsingi tusingetarajia kuona fedheha na aibu hii
kubwa inayotukumba sisi leo hii Hapa
nchini Kwetu. Kuna wakati nilikua natazama taarifa ya habari nikaona habari
inayo onyesha watu wa Jamhuri ya watu wa SWITZILAND wakitoa msaada wa MADAWATI
katiaka shule Fulani ya msingi huko Dar-es-salaam. Jamani hivi ni kweli tumekosa
miti yakuweza kutupatia hayo madawati ambayo watoto wetu wanalizimika kukaa
kwenye sakafu na juu ya mawe wakati wakiwa madarasani waifundishwa?
Ufugaji wa nyuki. |
Huo ni mfano mdogo tuu unaonyesha ni jinsi
gani bado rasilimali za misitu hapa nchini hatufaidiki nazo ipasavyo.Maoni yangu na mapendekezo yangu ni
haya juu ya swala la ukosefu wa madawati mashuleni.
Kwa sasa
zipa shule nyingi za UFUNDI hapa Tanzania ambazo zinamilikiwa na serekali na
baadhi ya nyingine zinamilikiwa na taasisi binafsi na point ni kwamba Kuna
baadhi ya misitu mikubwa ambayo imekomaa na ambayo inaweza kutupatia mbao kwa
ajili ya kutengeneza madawati yakutosha.
Kwa nini serekali
isivune miti hiyo kwa mujibu washeria na ki sha kutumia ile sera ya “KATA MTI
PANDA MITI” ili kurudisha miti ambayo
imevunwa kwa ajili yakutengeneza madawati?
Inawezekana
kabisa kufanya hivyo na kisha mbao kupatikana ambapo mbao hizo zitipelekwa
katika vyuo vya ufundi ambapo wanafunzi wanaojifunza ufundi seremala
watatengeneza madawati hayo kama sehemu ya somo lao darasani. Ni matumaini yangu kila mkoa
vyuo hivi vya ufundi vinapatikana na jambo hili linaweza kufanikiwa kwa kiasi Fulani.
Serekali Kwa
kupitia wataalamu wa mambo ya misitu waandae miche yakutosha kwa ajili
yakupanda sehem zitakazokua zimevunwa miti hiyo.
Kwakufanya hivyo tutaondoa aibu na tatizo hili
la ukosefu wa madawati Katika shule zetu.
Yasije yakawa yale ya “Penye miti mingi hapana wajenzi.”
Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe ulie
chukua nafasi na muda wako kupitia makala zetu. Tafadhali ungana nami tena
katika makala zetu zinazotoka kila Mwisho wa wiki.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA:-
Francis Mawere
KWA HISANI
YA MAWERE MEDIA GROUP Ltd (MMGLtd)
MAWASILINO:
Email: mtokambali2015@gmail.com Phone no:
0767322193
No comments:
Post a Comment