Kwa mara ya kwanza jukwaa la Ballon D’or litapata ugeni mpya wakati
mshambuliaji wa kibrazil Neymar Dos Santos atakapoungana na wafalme
wawili wa tuzo hizo ambao wameitawala tuzo hiyo zaidi ya miaka 8 –
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi – itakapofika January 2016. Kama
isingekuwa siasa za soka basi mbrazil huyo angeweza kushika nafasi ya
pili nyuma Lionel Messi. Lakini hii ni ‘era’ mpya ya soka.
Katika
miaka 8 iliyopita Ballon D’or imekuwa inatawalia na Messi dhidi ya
Ronaldo, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda inaonekana mtu wa
kupambana na Messi si Ronaldo tena ambaye umri unamtupa – anakaribia
kutimiza miaka 31, Ni Neymar ambaye nyota yake inazidi kung’aa kila
kukicha.
Pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri na washambuliaji
wengine wa Barca, pia Neymar ameonyesha anaweza ku-control mechi kama
ilivyo kwa Messi, tofauti na Ronaldo.
Wadau na wachambuzi wengi wa michezo duniani wanaamini katika kipindi
kifupi kijacho Neymar atakuja kuwa mwanasoka bora zaidi duniani, mimi
nikiwepo kwenye kundi hilo na hizi ndio sababu zangu.
- Kupafomu vyema Anapokosekana Messi
Unapocheza
pembeni ya Lionel Messi, vitu huenda kiurahisi zaidi. Wakati Messi
alipoumia hivi karibuni kwa zaidi ya mwezi mmoja, wachambuzi wengi
walikuwa na mashaka na uwezo wa Neymar kuziba pengo na kuisadia
Barcelona kama ilivyokuwa kwa Messi. Lakini matokeo yake, Neymar
akafanya vizuri zaidi katika kuisadia Barcelona kushinda kila mara na
sasa wapo juu ya kilele cha msimamo wa ligi na wamefuzu raundi ya 16
bora wa UEFA Champions League. Kuziba pengo la mmoja wa wanasoka bora
zaidi kuwahi kuugusa mpira sio jambo rahisi kabisa lakini kwa namna
Neymar alivyohimili presha na kuifanya kazi, inaonyesha wazi dalili za
world class player mwenye uwezekano wa kutwaa Ballon d’Or hivi
karibuni.
- Uwezo Binafsi
Yes,
ni kweli hivi sasa Neymar amekuwa mchezaji anayecheza kitimu zaidi
kuliko ilivyokuwa zamani. Hata kuna wakati timu ikiwa inacheza vibaya,
Neymar amekuwa akijitokeza na kuchukua majukumu ya timu kutumia uwezo
binafsi kuiletea timu matokeo chanya. Anaweza kuchukua ‘vijiji’
kiurahisi na kuiletea madhara makubwa ngome ya timu pinzani, si rahisi
kutabiri nini atafanya wakati mwingine. Ni mchezaji ambaye ni vigumu
kumkaba na mbinu zake kali alizonazo miguuni na kadri anavyoendelea
kucheza na kupata uzoefu, Neymar yupo njiani kuwa mwanasoka bora zaidi
duniani.
3. Uwezo wa Kuwachezesha Wenzie
Baadhi
ya wachezaji bora duniani wamekuwa bora kutokana na ukweli kwamba wana
uwezo wa kuwachezsha wachezaji wenzao. Mchezo wa Neymar huko nyuma
ulikuwa umeegemea katika uwezo wake binafsi zaidi na kuna muda alifanya
iwe rahisi kwa wapinzani kuzuia dhidi ya timu yao. Lakini kadri siku
zinavyozidi kwenda amekuwa sehemu muhimu ya timu, Neymar ameuelewa zaidi
mfumo na sasa anawachezsha mpaka wachezaji wenzie. Takwimu zinaonyesha
hivi sasa anapiga sana pasi kuliko ilivyokuwa zamani, hili la kupiga
pasi limeongeza kutokutabirika kwa mchezo wake na kuzidi kuwapa wakati
mgumu wanaomzuia kumkaba. Hili limeleta mabadiliko makubwa katika staili
ya uchezaji wa Neymar – pia limemletea mafanikio kuliko mwanzoni.
- Influence in the International side :
Wanaompinga
Neymar wana utetezi wao kwamba mchezaji huyo anafanya vizuri Barcelona
kutokana na sapoti ya Messi na Suarez lakini kiwango cha Neymar
kinapoangaliwa kwenye level ya timu ya taifa – ushahidi unaonyesha
Neymar ndio msingi mkuu wa mashambulizi ya timu ya Selecao. Nahodha huyo
wa Brazil ameitawala safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na ameiongoza
kimafanikio mpaka sasa akiwa na miaka 23 tu. Bado ana safari ndefu
kuendelea kuwa na kiwango kikubwa alichonacho. Ameyabeba majukumu ya
unahodha vizuri sana na anaamini hivi karibuni ataipa mafanikio Brazil.
5. Kawaacha Mbali Waliokuwa Wanashindanishwa Nae
Mbrazil
huyu amekuwa kiwango cha juu sana msimu uliopita na zaidi msimu huu.
Unapojaribu kumlinganisha na wachezaji wa kizazi chake kama Eden Hazard,
Antoine Griezmann, Gareth Bale utofauti wa uelewa wa mchezo na kukua
kwa Neymar. Anausoma mchezo vyema zaidi kuliko alivyokuwa Santos, anajua
wapi anatakiwa kukimbia na mpira na wapi kwa kupasia na hazidishi
manjonjo kama ilivyokuwa mwanzoni. Uhamisho wake kwenda Barcelona
umemsaidia katika kukua kiuchezaji na kuboreka zaidi katika mchezaji
hatari zaidi, hizi ni ishara halisi za mchezaji mwenye ubora wa kuwa
bora duniani.
No comments:
Post a Comment