04 February, 2016

Makamanda wa juu wa wanamgambo wa Islamic State wameingia nchini Libya


Makamanda wa juu wa wanamgambo wa Islamic State wameingia nchini Libya miezi ya karibuni wakitokea Iraq na Syria,Afisa wa maswala ya intelijensia nchini Libya ameeleza.
Afisa huyo ameliambia Shirika la utangazaji la uingereza  BBC kuwa wapiganaji wa kigeni wameingia mjini Sirte.
Wawakilishi kutoka nchi 23,wakiwemo wa kutoka Marekani na Uingereza wamekutana Rome siku ya jumanne kujadili tishio la wanamgambo wa IS nchini Libya.
Hali ya kutokubaliana kwa serikali hasimu nchini humo imesababisha jitihada za kupambana na IS kugonga mwamba.
IS iliudhibiti mji wa Sirte mwaka jana.mji huo ulikuwa makazi ya aliyekuwa Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Kundi la IS linaaminika kuungwa mkono na wale waliokuwa watawala wa utawala uliopita.
Lakini Ismail Shukri, mkuu wa idara ya intelijensia mjini Misrata, ameiambia BBC kumekuwa na wapiganaji wengi wa kigeni miezi ya karibuni.
Wengi wa wapiganaji wa IS ni wageni kwa asilimia 70. Wengi wao ni raia wa Tunisia,wakifuatiwa na Misri, raia wa Sudan na wachache kutoka Algeria.
Pia Raia wa Iraq na Syria, raia wengi wa Iraq wanatoka kwenye jeshi la Saddam Hussein.
Shukri amesema makamanda wa IS wamekimbilia Libya,kutokana na matukio ya mashambulizi ya anga nchini Iraq na Syria.
Mamlaka mjini Misrata zimesema zinajiandaa kupambana na IS mjini Sirte.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...