10 February, 2016

Donald Trump na Bernie Sanders wamepata ushindi katika mchujo wa jimbo la New Hampshire.

Trump
Seneta wa Vermont Bernie Sanders, aliyemshinda Hillary Clinton, amesema ushindi wake unaonesha watu wanataka “mabadiliko kamili”.
Bw Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala.
Maafisa wa jimbo walikadiria kwamba watu wengi wangejitokeza kushiriki kura za mchujo huo wa New Hampshire.
Gavana wa Ohio John Kasich alimaliza wa pili katika chama cha Republican, mbele ya gavana wa Florida Jeb Bush, Texas Seneta Ted Cruz na Seneta wa Florida Marco Rubio wote ambao wanang’ang’ania nafasi ya tatu.
Bi Clinton tayari amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kira kura kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.
Mchujo huo wa New Hampshire umewapa washindi nguvu mpya wanapoelekea kwa michujo ijayo South Carolina na Nevada.Trump
Ushindi wa Trump New Hampshire ndio wa kwanza mfanyabiashara huyo kutoka New York, ambaye hajawahi kuwania wadhifa wowote wa siasa, na ambaye amekuwa akiongoza kwenye kura za maoni.
Akitangaza ushindi wake, bilionea huyo amempongeza mshindi wa Democratic Bw Sanders lakini akamshambulia akisema “anataka kuuza taifa letu, jameni!”
Baada ya asilimia 50 ya kura kuhesabiwa, Seneta Sanders anaongoza kwa zaidi ya asilimia 10 ya kura dhidi ya Clinton.
Aliongoza kwenye kura za maoni New Hampshire kwa miezi kadha, na ilitarajiwa kwamba angeshinda, lakini bado ni ufanisi mkubwa.
Wengi wanaamini huenda ushindi wake umechangiwa na hali kwamba anatoka jimbo jirani la Vermont.Sanders
"Kile watu hapa wamesema ni kwamba ukizingatia mgogoro wa kiuchumi unaokabili nchi yetu kwa sasa, muda umepita kwa watu wale wale, ambao wamekuwa kwenye mfumo wa siasa na uchumi,” Bw Sanders alisema akiwahutubia wafuasi wake kwenye hotuba ya ushindi baadaye Jumanne.
Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 74 ameahidi kumaliza pengo kati ya matajiri na maskini, kutoa elimu ya vyuo vikuu bila malipo na ‘kuvunja’ benki kubwa kubwa

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...