Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.
Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa dalili zinaonyesha kwamba atakuwa wa pili.
Seneta wa Florida Marco Rubio anaonekana kufanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na huenda akamaliza nambari tatu.
Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.
Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.
Duru za karibu na mgombea wa Democratic Martin O'Malley, aliyekuwa gavana Maryland, zimeambia BBC kwamba atasitisha kampeni yake, na kufanya ushindani mkali sasa kuwa kati ya wagombea wawili.
Upande wa Republican, gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee ameandika kwenye Twitter kwamba atasitisha kampeni yake.
No comments:
Post a Comment