24 February, 2016

Wagombea urais wa chama cha Republican washindania jimbo la Nevada

Trump
Wagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wanakabiliana kwenye uchaguzi wa mchujo katika jimbo la Nevada katika kinyang’anyiro cha nne cha kuamua mgombea wa chama hicho.
Mfanyabiashara Donald Trump, ambaye amekuwa akiongoza kwenye kura za maoni kitaifa, anaongoza pia kwenye kura za maoni jimbo hilo, na anatarajia kupata ushindi wa tatu mtawalia baada ya kushinda New Hampshire na South Carolina.
Nevada, ambalo ni jimbo lisilo na mbabe na lenye watu wengi wa asili ya Amerika Kusini, ni muhimu sana katika uchaguzi.
Upigaji kura kwa sasa unaendelea na kuna foleni ndefu vituoni.
Kura ya maoni ya karibuni CNN/ORC imeonesha Trump ana uungwaji mkono 45% akifuatwa na Seneta Marco Rubio 19% naye Seneta Ted Cruz akiwa na 17%.
Ingawa Nevada ina wajumbe wachache, inatarajiwa kuwa mtihani kwa Trump kutokana na matamshi yake dhidi ya wahamiaji ikizingatiwa kwamba ina watu wengi wa asili ya Amerika Kusini.
Hillary Clinton alishinda kwenye jimbo hilo katika chama cha Democratic Jumamosi.
Alimshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa kumpita kwa asilimia tano na wagombea hao wawili sasa wanaangazia jimbo la South Carolina lenye watu wengi weusi.
Uchaguzi wa mchujo wa chama cha Republican katika jimbo la South Carolina utafanyika Jumamosi.
Uchaguzi wa mchujo hutumiwa kuchagua wagombea wa vyama viwili vikuu kwenye uchaguzi mkuu wa urais ambao utafanyika mwezi Novemba

 SOURCE: BBC

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...