01 February, 2016
Marekani kutowa msaada zaidi kwa Ethiopia kukabiliana na ukame
Idara ya misaada ya maendeleo ya Marekani USAID, imetangaza kutowa dola millioni 97 ya msaada wa dharura kwa Ethiopia kusaidia kukabiliana na mzozo unaoendelea wa kibinadam, ulosababishwa na athari za mfumo wa El Nino.
Serikali ya Marekani inasaidia waethopia kukabiliana na athari za El Nino na msaada wetu wa ziada utasidia kujenga juhudi za kushugulikia hali hiyo inayoendelea, alisema mratibu wa USAID Gayle Smith, katika taarifa ilotolewa jana.
Idara ya USAID inaeleza kuwa hali ya jotojoto ilotanda katika bahari ya Pacific, imeathiri kwa kiasi kikubwa mifumo ya hali ya hewa , na kuharibu uzalishaji wa kilimo, na kufanya maisha kuwa magumu, na kadhalika usalama wa chakula miongoni mwa watu masikini na dhaifu.
USAID inaeleza kuwa msaada huo unajumlisha zaidi ya tani elfu 176 ya chakula ambacho kitasambazwa kwa waethiopia na wakimbizi takriban millioni nne.
Katibu mkuu wa umoja mataifa Bw Ban Ki Moon, alionya jana kuwa Ethiopia inakumbwa na ukame mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30. Alisema, kiwango cha dharura kinachokabiliwa na Ethiopia ni kikubwa mno kwa taifa moja kuweza kukabiliana nayo pekee yake.
Umoja mataifa unaeleza kwamba watu millioni 10 wanahitaji chakula huko Ethiopia, na kuongezea kuwa, idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu katika kipindi cha miezi 9.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment