13 February, 2016

Naibu Rais wa Kenya William Ruto amepata ushindi Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)

Ruto
Naibu Rais wa Kenya William Ruto amepata ushindi muhimu kwenye kesi yake inayosikizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) baada ya majaji wa rufaa kukubali rufaa yake ya kupinga kutumiwa kwa ushahidi wa mashahidi waliojiondoa.
Hii ina maana kwamba ushahidi ulioandikishwa awali na upande wa mashtaka hauwezi kutumiwa dhidi ya Bw Ruto na mwanahabari Joshua Sang.
Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa upande wa mashtaka unaoongozwa na Fatou Bensouda.
Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita waliokuwa wanahusisha Bw Ruto na ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-08, vilivyosababisha vifo vya watu 1,200, walioondoa ushahidi wao.
Upande wa mashtaka unasema walitishiwa au wakahongwa.
Majaji wa rufaa wamebatilisha uamuzi wa awali wa majaji uliosema upande wa mashtaka unaweza kutumia ushahidi uliowasilisha na mashahidi hao kabla yao kubadili nia.
"Ushahidi ulioandikisha awali uliwasilishwa bila washtakiwa kupewa fursa ya kuwahoji na kuwauliza maswali mashahidi hao,” amesema jaji wa mahakama ya rufaa Piotr Hofmanski.
Bw Sang amefurahia uamuzi huo na kusema maombi yake yamejibiwa.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...