Mwanamke aliyekataa
matibabu ya figo kuokoa maisha yake nchini Uingereza, akisema
ameshapoteza mng’ao, amefariki. Mwanamke huyo wa umri wa miaka 50
aliyetambuliwa tu kama C, aligonga vichwa vya habari baada ya jaji
kuamua kwamba ana haki ya kukataa kupokea matibabu ya kusafisha damu.
Figo za C ziliharibika baada yake kunywa dawa kupita kiasi akitaka
kujiua. Mahakama iliambia kwamba katika maisha yake, C aliangazia zaidi
"sura yake, wanaume na vitu vya thamani.”
Mmoja wa bindi zake aliambia mahakama: “Kupona kwake si kwamba figo zake
zianze kufanya kazi tena pekee, bali atahitaji kupata ‘mng’ao’, jambo
ambalo anaamini hawezi kuapata tena kutokana na umri wake.”
Mwaka uliopita, C alikuwa amepatikana na saratani ya matiti lakini
akakataa matibabu akisema matibabu hayo yangemfanya kuwa mnene.
Baada ya kupata matatizo ya figo, wakfu wa Huduma ya Taifa ya Afya
Uingereza katika hospitali ya King’s College ulitaka alazimishwe kupokea
matibabu. Lakini Jaji MacDonald, kwenye uamuzi alioutoa Novemba 13,
alisema C ana uhuru wa kufanya uamuzi.
House of Entertainment, News, Gossip, Music and Videos!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment