Utafiti mmoja uliofanywa nchini China umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu.
Utafiti huo haswa umeonesha kuwa ukila chakula hususan pilipili utaishi maisha marefu zaidi duniani.
Watafiti mjini Baijing walidadisi maisha na vyakula wanavyokula wenyeji nusu milioni katika kipindi cha utafiti cha miaka 7.
Utafiti huo ulibaini kuwa wale waliokula chakula kilichojumuisha
pilipili walikuwa katika hali bora zaidi kiafya wala hawakuwa katika
hatari ya kuaga dunia. Hali yao ya siha ilitofautiana sana
ikilinganishwa na wale ambao waliweka viungo katika vyakula vyao chini
ya siku moja kwa juma .
Watafiti hao walitoa tahadhari.
Wanasema kuwa utafiti huo ulikuwa wa ushahidi tu lakini wakashauri
utafiti zaidi ufanyika kwengineko ilikutilia pondo utafiti wao.
Hata hivyo walibaini kwa uhakika kuwa kiungo kinachopatikana katika
pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana na seli zinazotuma ujumbe
kwa ubongo kuwa mtu amezeeka na kusababisha viashiria vya utu uzima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment